Mahadh aikosa St. Louis

Muktasari:

  • Yanga itacheza mfumo wa 3-5-2 ambao mara kwa mara timu inayoutumia hutawala eneo la kiungo.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadh ataukosa mchezo wa baadaye dhidi ya St. Louis kutokana na kusumbuliwa na tatizo la mafindofindo.

Mahadh alianza kuugua ghafla usiku wa kuamkia jana ambapo alipatiwa matibabu na kumfanya akose mazoezi ya asubuhi lakini bado ameshindwa kuwa katika hali nzuri ya kucheza.

Kutokana na kukosekana kwa Mahadh, Kocha George Lwandamina amelazimika kufanya mabadiliko ya kimbinu kwa kujaza idadi kubwa ya viungo kwenye kikosi chake kwa lengo la kutowapa nafasi wapinzani wao kumiliki mpira.

Yanga itacheza mfumo wa 3-5-2 ambao mara kwa mara timu inayoutumia hutawala eneo la kiungo