Yanga kuwazadia mashabiki taji la kwanza SportPesa Cup

Muktasari:

  • Matarajio ya uongozi wa Yanga ni kwamba wachezaji watapambana kufa na kupona ili kuhakikisha wanacheza na Everton jambo ambalo litawasaidia nao kujitangaza kimataifa.

Dar es Salaam. Uongozi wa Yanga umesema sasa ni zamu ya klabu hiyo kuhakikisha inawapa zawadi mashabiki wao kwa kuhakikisha inalibakisha kombe la SportPesa nyumbani.

Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaaya Yanga ilisema kutokana na kuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa hawatarajii kuwa na visingizio. Pia matarajio yao makubwa ni kwamba wachezaji watapambana kufa na kupona ili kuhakikisha wanacheza na Everton jambo ambalo litawasaidia nao kujitangaza kimataifa.

Kaaya alisema kwamba licha ya kila upande kuvutia upande wake kuwa itafanya vyema, lakini bado anaamini mpira ni dakika 90.


Mashindano hayo yanatarijiwa kuhusisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya. Timu kutoka Tanzania ni Simba, Yanga, Singida Unted, pamoja na Mbao FC ambao watakakuwa wenyeji wa Mkoa wa Mwanza.

Katika mashindano yaliyopita klabu ya Simba ilifika hatua ya fainali na kucheza dhidi ya Gor Mahia nchini Kenya, mchezo ambao Gor waliibuka kidedea kwa mabao 2-0 na kuwapa nafasi ya kuzuru kwenye dimba ya Godson Park hivi karibuni.

Hata hivyo katika mchezo huo vijana wa Everton waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.