Thursday, September 14, 2017

Yanga sasa kamili gado

 

By Gift Macha

Njombe. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga sasa wako imara kuikabili Majimaji ya Songea baada ya kumaliza kambi yake hapa Njombe.

Mabingwa hao wameondoka leo asubuhi Alhamisi kwenda Songea wakati ambapo kocha, George Lwandamina akiwa amefanyia kazi changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye mchezo uliopita.

Katika mazoezi ya jana jioni mjini hapa, Lwandamina alifanya kazi kubwa kuwanoa nyota wake katika eneo la kufunga.

"Tunahitaji kuwa na matokeo mazuri, hivyo lazima tuendelee kutazama mbele kwa kurekebisha changamoto zilizojitokeza," alisema Lwandamina.

-->