Yanga wamerudi kivingine, mashabiki jiandaeni kushangilia!

Muktasari:

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema wamemaliza mgomo waliouweka wachezaji hao na leo Jumatano walifanya mazoezi kama kawaida katika Uwanja wa Uhuru.

KIKOSI cha Yanga kimemaliza mgomo wa siku moja waliouweka jana Jumanne kwa kugomea mazoezi kutokana na kuwa na malimbikizo ya mishahara na posha za baadhi ya mechi ingawa wenyewe hawakutaka kuweka wazi.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema wamemaliza mgomo waliouweka wachezaji hao na leo Jumatano walifanya mazoezi kama kawaida katika Uwanja wa Uhuru.

“Tulikuwa kwenye kikao jana cha muda mrefu na tumeingia makubaliano na wachezaji na tumekubaliana kila kitu na ndio maana leo wamefanya mazoezi kama kawaida,” alilisema Ten.

Kikosi hicho kamili leo Jumatano asubuhi walifanya mazoezi kwenye uwanja wa Uhuru kujinoa na mchezo wao na Ndanda wikiend hii.