Yanga yatibua hesabu za Mrundi kutwaa ubingwa

Thursday November 9 2017

 

By Thobias Sebastian

Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma amesema katika timu ambazo amezitazama kwenye runinga na zinaweza kuwa kikwazo kwao msimu huu, ni Yanga licha ya kwamba sasa wameiacha alama mbili.

“Yanga ina wachezaji wazuri wa kimataifa tena wenye majina makubwa na uwezo. Siyo timu ya kuibeza kabisa hata kama wameanza ligi kwa sare nyingi muda wowote wanaweza kubadilika,” alisema.

“Timu nyingine ambazo zimeanza vizuri na nimeziona kuwa zinaweza kufanya vizuri ni Azam hawa nilikuwa nikiwasikia kabla ya kuja hapa nchini, lakini Mtibwa nao wameanza vizuri na wanastahili kuwepo katika timu za juu kwenye msimamo wa ligi,” alisema.

 

Advertisement