Yanga yatua kwa balozi

Muktasari:

Yanga imefuzu kwa mara ya pili kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika

Hawassa, Ethiopia. Kikosi cha Yanga kimeanza safari ya kutoka  Hawassa kuelekea jijini Addis Ababa ambapo mchana wa leo kitakula chakula cha pamoja na balozi wa Tanzania nchini Etgiopia.

Yanga jana jioni ilikata tiketi ya kushiriki hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kuwaondoa Welayta Dicha kwa jumla ya mabao 2-1 licha ya mchezo ya kupokea kipigo cha bao moja kinakwenda kwa balozi kufuatia mualiko maalum.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hamad Islam ameondoka na timu hiyo asubuhi Hawassa amesema wamepokea simu kutoka kwa balozi akiitaka timu hiyo kufika nyumbani kwake kuwapa mkono wa pongezi.

Islam alisema ikiwa hapo Yanga itapata chakula cha mchana na kuagana na balozi kabla ya kuanza safari ya kurudi nyumbani wakipitia Kenya na kutua jijini Dar es Salaam saa saba usiku.

"Mheshimiwa balozi ametuita kwake kutupa mkono wa pongezi baada ya mafanikio ya jana, unajua hakupata nafasi ya kuja uwanjani, lakini sasa amesema angalau akawapongeze vijana pale kwake," alisema Islam.

"Tukiwa pale ataongea na vijana kidogo lakini ilikuwa tuate chakula hapa Hawassa ametuzuia akitaka tupate chakula hicho tukiwa naye tukimaliza hapo jioni tutaanza safari ya kurudi nyumbani tukipitia Kenya na tunataraji kufika nyumbani Tanzania saa saba usiku."