Zidane agoma kumzungumzia Neymar

Saturday November 18 2017

 

Madrid, Hispania. Zinedine Zidane amekataa kuzungumzia uwezekano wa Neymar kujiunga Real Madrid wakati timu yake ikijiandaa na mechi ya watani wa jadi wa jiji la Madrid, Atletico Madrid leo jioni.
Mshambuliaji huyo wa Brazil amekuwa mchezaji ghali zaidi wakati alipoondoka Barcelona na kujiunga na Paris Saint-Germain msimu huu.
Hata hivyo, taarifa zinamuhusisha nyota huyo mwenye miaka 25, kutaka kurejea Hispania lakini sasa ikiwa ni Santiago Bernabeu, na Zidane ameonyesha lolote linaweza kutokea kwa siku za baadaye.
"Neymar ni mchezaji mzuri, hilo halina ubishi," alisema Zidane wakati alipokuwa katika mkutano kuzungumzia mechi ya leo dhidi ya Atletico.
"Nina wachezaji wazuri hapa ndiyo nilikuwa katika kikosi change. Unaweza kufanya kazi na wachezaji uliokuwa nao hapa. Mambo ya baadaye nani anayejua?"
Neymar ameisaidia PSG kuongoza katika msimamo wa Ligue 1, akiwa amefunga mabao saba katika michezo nane.

Advertisement