Dogo Janja afunguka mtoto nje ya ndoa

Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Abubakar maarufu Dogo Janja.

Muktasari:

  • Dogo Janja ambaye ni mume wa mcheza filamu, Irene Uwoya ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Agosti Mosi, 2018 akizungumza katika kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha East Africa.

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Abubakar maarufu Dogo Janja amesema hawezi kupelekewa mtoto wa nje.

Dogo Janja ambaye ni mume wa mcheza filamu, Irene Uwoya ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Agosti Mosi, 2018 akizungumza katika kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha East Africa.

Amesema haiwezekani akatokea msichana na kudai kuwa ana mtoto wake.

Dongo Janja amesema kauli yake inatokana na umakini wake katika uhusiano wake wa huko nyuma, akisisitiza kuwa alikuwa akitumia kinga.

Amesema pia anazingatia ushauri wa baba yake mzazi aliyemsihi kutothubutu kuwa na mtoto kabla ya kuoa.

“Katika vitu nilivyokuwa makini katika mahusiano yangu ni kutumia kinga. Hakuna mtu atakuja kuniambia kuwa ana mtoto wangu na mimi ndiye baba. Uwoya pekee akieleza kuwa na mtoto wangu ndio ataeleweka kwa kuwa nipo naye kwa sasa,” amesema Dogo Janja.