VIDEO- Ommy Dimpo aweka hadharani ugonjwa unaomsumbua

Muktasari:

  • Akizungumza na mchambuzi wa soka Edo Kumwembe akiwa nyumbani kwakwe nchini Afrika Kusini, Dimpoz alisema kwamba alifanyiwa operesheni ya koo baada ya kushindwa kula chakula na kumeza maji.

Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpo ameweka hadhani ugonjwa unamsumbua, jambo ambalo limesababisha afanyiwe operesheni ya koo.

Akizungumza na mchambuzi wa soka Edo Kumwembe akiwa nyumbani kwakwe nchini Afrika Kusini, Dimpoz alisema kwamba alifanyiwa operesheni ya koo baada ya kushindwa kula chakula na kumeza maji.

Alisema kwamba wakati mwingine chakula kilikuwa kinakwama kushuka hivyo alilazimika kufanya vipimo vya awali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Pia alifanikiwa kwenda Mombasa nchini Kenya ambako alishauriwa na madaktari wa huko kwenda kufanyiwa matibabu zaidi Afrika Kusini.

Amesema hata hivyo baada ya kufanyiwa operesheni kwa sasa anaendelea vyema na anaweza kula tofauti na hali ilivyokuwa awali.

Ommy Dimpoz amesema anawashukuru Watanzania waliokwenda kumfariji akiwa hospitali na nyumbani Afrika Kusini.

Pia aliwatoa hofu mashabiki wake kwamba licha ya kuugua kwa kipindi kirefu, lakini ameshapika vibao vingi ambavyo amevihifadhi na atakaporejea kwenye hali ya kawaida ataingia studio kwa ajili ya kurekodi video.

Alisema tukio la kuugua kwake halijafahamika na wengi kutokana na kuliweka jambo hilo kuwa la kifamilia. Hata hivyo aliwashtua  mashabiki wake baada ya kuposti Istagram kuhusu hali yake kwamba anaendelea vizuri.

Hakikisha unasoma gazeti la Mwanaspoti kuanzia Jumatatu, Juni 18 ambapo Dimpoz ameeleza kila kitu katika mahojiano maalumu na Edo Kumwembe.