VIDEO: Papi Kocha anogesha uzinduzi Bogoss

Muktasari:

  • Mwanamuziki papii Kocha kupanda jukwaani na kuimba wimbo wa Seya na wanamzuiki wa Bogoss, huku akimshukuru Rais John Magufuli na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publisher, Eric Shigongo,huku kuwatupia madogo waliomfunga jela.

Katika uzinduzi wa Bogoss jana Jumamosi, kivutio kikubwa kilikuwa ni muonekano wa waimbaji wa Bendi ya Bogoss ni vijana na wanauwezo wa kupangilia sauti ya kwanza hadi ya tatu.

Mwanamuziki papii Kocha kupanda jukwaani na kuimba wimbo wa Seya na wanamzuiki wa Bogoss, huku akimshukuru Rais John Magufuli na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publisher, Eric Shigongo,huku kuwatupia madogo waliomfunga jela.

Nyoshi El saadat kuwatambulisha watoto wake wawili kati ya kumi na mbili aliokuwa nao.

Nyoshi alimtambulisha mtoto wake wa kwanza wa kiume mwenye umri wa miak 19,aliyezaa na marehemu Rukia Bruno, na baadae alimtambulisha mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 18 aliyezaa na Amina Rusha roho.

Kivutio kingine ni pale Nyoshi kutoa shukrani kwa wanahabari,wadau wa muziki wa dansi, viongozi wa Basata kwa kumpa sapoti katika bendi yake ya Bogoss,huku akisisitiza kuwa yeye ni shemeji yao.

Pia katika sekta ya wapiga vyombo nao walikuwa kivutio kukumbini humo amboa ni, mpiga dramu Bala Telly, Decatobanse mpiga bass, Topaz Alqaida mpiga Dram,Kichinja Elombee mpiga Solo,Kaposhoo Mpiga tumba.