Tamasha la SexTour lampeleka Idris Sultan Sauzi

Muktasari:

  • Tamash la SexTour lilidhaminiwa na Mfuko wa dharura wa Raisi wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya Ukimwi (PEPFAR) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani Tanzania.

Dar es Salaam. Mchekeshaji Idris Sultan atahudhuria tamasha kubwa la Komedi litakalofanyika nchini Afrika Kusini, moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji lililoandaliwa na Comedy Central.

Mualiko wa Idris unakuja baada ya msanii huyo wa tasnia ya uchekeshaji kufanya Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu ya wapenzi wa comedy hapa nchini.

Kwa mujibu wake mualiko wa huo ni sifa kubwa kwa Taifa, baada ya bongo flava kutoboa kimataifa, sasa ni zamu ya tasnia ya uchekeshaji wa Tanzania.

Akizungumzia kuhusu tamasha la Sex Tour Idris alisema lilikuwa na lengo kuu ya kuburudisha na kuelimisha watu katika ma suala mbalimbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji.

“Tarehe 1 Desemba Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la SexTour katika ukumbi wa Next Door Arena. Watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa tiketi.”

“SexTour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa ya muziki” anasema

Tamasha hilo lilibeba ujumbe "Kutokupima hakubadili matokeo"tamasha hilo lilihudhuriwa na  wachekeshaji mbalimbali akiwemo Jaymondy, Mkaliwenu,  Dogo pepe, Coy Mzungu, Blackpass, kitenge, Nalimi ,Optalema Deo, Max, Young Unstopable, D comic na wengine wengi huku upande ma muziki wa kizazi kipya ukiwalishwa vyema naa Whozu na Billnass

“Changamoto za maambukizi mapya kwa vijana wa umri 15-24 bado ni kubwa, hivyo Sex Tour ilikua inalenga zaidi kushauri vijana kujali afya zao, kutokuwa na hofu ya kupima afya zao lakini pia kubadili fikra potovu za kuwa nyanyapaa wenye maambukizi,”anasema Idris

Tamash la Sex Tour lilidhaminiwa na Mfuko wa dharura wa Raisi wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya Ukimwi (PEPFAR) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani Tanzania.