Wikiendi uende wapi?

Muktasari:

  • Katika Ukumbi wa Dar Live, Juni 16 mwanamuziki Harmonize, akisindikizwa na Queen Darlin, Dula Makabila, Walidy watawasha moto katika Usiku wa Kusi.

Kama upo Dar es Salaam, Juni 16 mwanamuziki Davido kutoka Nigeria atakuwa akitumbuiza katika kiwanja kipya cha Nextdoor Arena akisindikizwa na The Mafik, Ruby na Nandy.

Katika Ukumbi wa Dar Live, Juni 16 mwanamuziki Harmonize, akisindikizwa na Queen Darlin, Dula Makabila, Walidy watawasha moto katika Usiku wa Kusi.

Mint Club

 Wapi- Bukoba

Kama upo Bukoba wikiendi hii unaweza kupunguza uchovu wa kazi wa wiki nzima kwa kujirusha Mint Club kuanzia leo Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

 

Ambassador

Kama upo ndani ya Mji wa Geita  kiwanja hiki kipo katika barabara ya kuelekea mgodi mkubwa wa dhahabu. Ukiwa kwenye Club ya Ambassador utapata chakula kizuri,mchemsho wa ndizi samaki fresh na kuku.