#WC2018: Kocha Hispania: Ronaldo si mtu mzuri

Muktasari:

  • Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Hispania, Fernando Hierro, amesema hakushangaa kumuona Cristiano Ronaldo, akiifungia Ureno mabao matatu ‘hat trick’ timu hizo zilipokutana jana usiku katika mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia.

Moscow, Russia. Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Hispania, Fernando Hierro, amesema hakushangaa kumuona Cristiano Ronaldo, akiifungia Ureno mabao matatu ‘hat trick’ timu hizo zilipokutana jana usiku katika mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia.

Hierro amekiri kuwa Ronaldo anatisha na ameithibitishia Dunia kuwa ni mchezaji wa kiwango cha juu katika mchezo huo wa Kundi B ulioisha kwa sare ya mabao 3-3.

“Ninajivunia wachezaji wangu kwa hakika wamefanya kazi kubwa kumdhibiti Ronaldo, huyu ni mchezaji anayetisha kwa kweli, binafsi sikumuandaa mtu maalum wa kumdhibiti kwa sababu ninajua wote wanamfaham na niliamini watamdhiti lakini ikawa tofauti walishindwa kumzuia,” alisema.

Hiero alisema kutokana na kile alichokionyesha Ronaldo ni wazi kuwa atafanya makubwa zaidi katika mechi zijazo za fainali za Kombe la Dunia.

Alimfagilia Ronaldo akisema ni mchezaji mwenye kujituma na kupambana kwa ajijili ya timu na kwamba mambo huwa mazuri dimbani anapokuwepo mchezaji kama huyo.

Katika mchezo huo uliopigwa mjini Sochi, mabao mawili ya kwanza ya Ronaldo yaliifanya Ureno kuongoza kabla ya Diego Costa kuifungia Hispania mabao ya kusawazisha na Nacho Fernandez akaipa Hispania bao la kuongoza lakini Ronaldo akaisawazishia Ureno kwa mpira wa adhabu.

Hierro aliwataka mashabiki kutomlaumu kipa David De Gea kutokana na bao la pili alilofungwa na Ronaldo kwa shuti la mbali lililojaa wavuni.