Simba yaijazia KVZ mastaa Kombe la Muungano Simba imeweka hadharani kikosi chake kitakachoanza dhidi ya KVZ kwenye Kombe la Muungano muda mfupi ujao katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar huku ikiwa na kundi kubwa la nyota wake.