#WC2018: Brazil wana utoto mwingi

Muktasari:

  • Brazil ni bingwa mara tano wa Kombe la Dunia

Kocha wa Brazil, Tite Coutinho, amepingana na wanaosingizia rafu kutoka kwa Uswisi, badala yake aliwashutumu vijana wake akisema walikosa ushindi hapo jana kutokana na kuendekeza utoto.

Kocha huyo alisema itakua vigumu kwao kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2018, iwapo vijana wake hawatabadilika, hata hivyo ameahidi kulifanyia kazi haraka ili lisijirudie.

Katika mechi yao ya kwanza ya kundi E, Brazil walibanwa kwa sare ya bao 1-1 licha ya kutangulia kufunga bao la kuongoza lililozamishwa na Philippe Coutinho, lakini wakaruhusu bao la kusawazisha lililofungwa na Steven Zuber, matokeo yaliyodumu hadi mwisho wa mchezo.

“Uswisi walicheza kwa nidhamu, wasiwasi na kujituma kwa dakika zote 90 za mchezo, walikaba kwa ushirikiano na walitushambulia kwa haraka, ni makosa kusema walicheza rafu sana bali walijituma, wakawazuia wachezaji kama Neymar wasilete madhara,” alisema Tite.

Kocha huyo ambaye ni mmoja wa magwiji wa soka nchini Brazil, alisema soka la sasa linahitaji nguvu na sio kucheza kwa mbwembwe nyingi ili kuwafurahisha watazamaji jukwaani kama walivyocheza vijana wake jana.

Alisema Brazil waliuanza mchezo huo kwa presha nzuri wakiwalazimisha wapinzani wao kufanya makosa yaliyowapa nafasi ya  kupata bao la kuongoza lakani baada ya hapo wakajisahau.

Baada ya sare hiyo na Uswisi, hivi sasa Brazil inaelekeza nguvu zake katika mechi dhidi ya Serbia na Costa Rica.