#WC2018: Uruguay kuamua hatima ya Mo Salah Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Nyota  Ronaldo, Diego Costa, Suarez kuingia mzigoni leo

Ushindi wa Russia wa mabao 3-1 dhidi ya Misri, umewapa mwanga wa kukaribia kutinga hatua ya timu 16 bora baada ya kufikisha pointi 6.

Leo Uruguay itakuwa na kibarua dhidi ya Saudi Arabia ambapo kwa sare au ushindi wa timu hiyo utakuwa umeipa nafasi Misri kurudi  nyumbani.

Wenyeji Russia na Uruguay watafuzu kwa hatua ya timu 16 za mwisho.

Hata iwapo Saudi Arabia itashinda, mabao ya Russia yanatosha kuiwezesha kufuzu.

Mechi za Jumatano 20/6/2018

Ratiba ya mechi siku ya Jumatano ni kama ifuatayo.

KUNDI B:

Ureno vs Morocco: Luzhniki Stadium, Moscow

KUNDI B: Iran vs Hispania:Kazan Arena, Kazan

KUNDI A:

Uruguay vs Saudi Arabia: Rostov Arena, Rostov-on-Don