-
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas (kulia) akiangalia nyara za serikali zilizokamatwa eneo la Mateves,Ngaramtoni ya Chini, jijini Arusha, jana katika nyumba ya mkazi wa eneo hilo. Habari kamili Uk3. Picha na Filbert Rweyemamu
-
Baadhi ya watuhumiwa wa vurugu zilizotokea Mbagala jijini Dar es Salaam na kusababisha baadhi ya makanisa kuvunjwa na kuchomwa moto, wakiwa chini ya ulinzi wa Askari Magereza katika Kanisa la Kiinjili la Kilitheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mbagala baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
-
Mkazi wa Buyekera katika manispaa ya Bukoba, Ishengoma Ernest akisubiri kumkabidhi Kakakuona kwa uongozi wa manispaa baada ya kumkamata jana. Kakakuona ni mnyama anayeaminika huweza kutabiri matyukio mbalimbali.Picha na Lilian lugakingira
-
Haneni Juma akikarabati spika za mziki kama alivyokutwa mwishoni mwa wiki katima mtaa wa Luswega mjini Morogoro. Vijana wengi wamekuwa wakitumia vipasji vyao ili kujiingizia kipato.Picha na Masoud Masasi
-
Mafundi wa kampuni ya ujenzi ya STRABAG inayojenga Barabara ya Morogoro wakiendelea na ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo kasi eneo la Manzese, Dar es Salaam, jana. Picha na Rafael Lubava
-
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bungo iliyopo Manispaa ya Morogoro, Roman Luoga akimfundisha namna ya kuandika namba mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule hiyo, Joyce Telephory (7) walipoanza kusoma jana baada ya kufunguliwa kwa shule hiyo. Picha na Juma Mtanda
-
Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa Igunga kwenye Uwanja wa Barafu mjini Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga, mkoani Tabora, jana. Picha na Ikulu
-
Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Musa Luhamba akitoa taarifa juu ya mchakato wa kununua mtambo wa kuchongea barabara (Motor Grader) ulionunuliwa na Halmashauri hiyo kwa gharama ya Sh581m. Picha na Hakimu Mwafongo
-
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi kituo cha kompyuta cha kanisa Anglikani Parishi ya Magugu kilichopo wilayani Babati Mkoa wa Manyara, juzi. Picha na Habel Chidawali
-
Mfanyabiashara katika Manispaa ya Morogoro akiwa na zambarau mara baada ya kuzinunua kutoka kwa vijana wanaochuma ili kuuza kwa wateja wake kwa Sh200 kwa kikombe.