Tuzo za soka Afrika zinaonyesha kile tulichopanda

Muktasari:

  • Katika tuzo zote, Tanzania hatumo hata moja!. Yaani katika tuzo ya mchezaji soka bora wa kike wa mwaka wa Afrika, timu bora ya wanawake ya mwaka, kocha bora wa mwaka, timu bora ya Taifa ya mwaka, mchezaji bora kijana wa mwaka, mwamuzi bora wa mwaka, mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017 na mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Afrika.

Tayari majina ya wachezaji, makocha, klabu, timu za Taifa na waamuzi watakaoshiriki katika kuwania tuzo mbambali za soka Afrika yameishafahamika na washindi watatangazwa katika sherehe zitakazofanyika Januari 4, 2018 mjini Accra, Ghana.

Katika tuzo zote, Tanzania hatumo hata moja!. Yaani katika tuzo ya mchezaji soka bora wa kike wa mwaka wa Afrika, timu bora ya wanawake ya mwaka, kocha bora wa mwaka, timu bora ya Taifa ya mwaka, mchezaji bora kijana wa mwaka, mwamuzi bora wa mwaka, mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017 na mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Afrika.

Walioingia katika tuzo hizo ni kama ifuatavyo: Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017: Bertrand Traore (Burkina Faso & Olympique Lyon), Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns), Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord), Keita Balde (Senegal & Monaco), Mohamed Salah (Misri & Liverpool), Naby Keita (Guinea & RB Leipzig), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & B. Dortmund), Sadio Mane (Senegal & Liverpool), Victor Moses (Nigeria & Chelsea), Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto) na Yacine Brahimi (Algeria & Porto).

Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Afrika: Achraf Bencharki (Morocco & Wydad Athletic Club), Ahmed Fathi (Misri & Al Ahly), Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly), Aristide Bance (Burkina Faso & El Masry), Ben Malango (DR Congo & TP Mazembe), Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns), Jeremy Brockie (New Zealand & Supersport), Junior Ajayi (Nigeria & Al Ahly), Mohamed Ounnajem (Morooco & Wydad Athletic Club) na Taha Yassine Khenisssi (Tunisia & Esperance).

Katika tuzo ya mchezaji soka bora wa kike wa mwaka : Asisat Oshoala (Nigeria & Dalian Quanjian), Chrestina Kgatlana (Afrika Kusini & UWC Ladies), Gabrielle Aboudi Onguene(Cameroon & CSKA Moscow), Rutendo Makore (Zimbabwe & Black Rhinos) na Tabitha Chawinga (Malawi & Kvarnsvedens).

Huku katika tuzo ya timu bora ya Taifa kwa upande wanawake zinazowania ni: Ghana U-20, Kenya, Nigeria U-20, Afrika Kusini na Zimbabwe. Kwa upande wa wanaume timu zinazowania tuzo ya timu bora za Taifa ni: Cameroon, Misri, Mali U-17, Nigeria na Zambia U-20.

Kwa upande wa kocha bora wa mwaka, wanaowania ni: Gernot Rohr (Nigeria), Hector Cuper (Misri), Hugo Broos (Cameroon), L’Hussein Amoutta (Wydad Athletic Club) na Mihayo Kazembe (TP Mazembe).

Katika tuzo ya klabu bora ya mwaka zipo: Al Ahly, Mbabane Swallows, SuperSport United, TP Mazembe na Wydad Athletic Club. Wakati katika tuzo ya mchezaji bora kijana wa mwaka wapo: Eric Ayiah (Ghana & Charity Stars), Krepin Diatta (Senegal &Sarpsborg), Luther Singh (South Africa & Braga), Patson Daka (Zambia & Liefering) na Salam Giddou (Mali & Guidars).

Mwisho, katika tuzo ya mwamuzi bora wa mwaka wanaowania ni: Bamlak Tessema (Ethiopia), Ghead Grisha (Misri), Janny Sikazwe (Zambia), Malang Diedhiou (Senegal), Mehdi Abid Charef (Algeria) na Papa Bakary Gassama (Gambia).

Kwa kuangalia washiriki waliopenya katika tuzo hizi za Afrika, angalau wenzetu wa Uganda wanae kipa Denis Onyango katika tuzo mbili (Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017 na tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani Afrika.