VIDEO: Mvua zaacha maelfu bila makazi Kilosa

MAFURIKO YAACHA MAELFU BILA MAKAZI KILOSA

Muktasari:

Maeneo mengi mkoani Morogoro yameaathirika na mvua hizo lakini wilaya ya Kilosa imeathirika zaidi kwa uharibifu wa miundombinu na nyumba za wananchi

Morogoro. Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha madhara makubwa mkoani Morogor huku wilaya ya Kilosa ikiwa imeathirika zaidi kufuatia kaya 1,734 zenye watu 6,298 kukosa makazi baada ya mafuriko kuharibu nyumba zao pamoja na madaraja, visima na barabara.

Akizungumza na wananchi kijiji cha Tindiga wilayani Kilosa, Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven asema kuwa mpaka sasa mvua zinaendelea kunyesha zimeleta athari kwa kusababisha miundombinu mbalimbali kuharibika.