Monday, March 20, 2017

Wabunifu majengo kuingizwa upya darasaniAmbwene Mwakyusa

Ambwene Mwakyusa 

By Aziza Nangw, Mwananchi

Dar es Salaam. Wahitimu wa kada ya wabunifu wa majengo na wakadiriaji wametakiwa kutoanza kazi kabla ya kupata mafunzo maalumu kutoka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ili kuboresha utendaji wao.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa amesema jana kwamba wahitimu hao watapata mafunzo na kupewa mtihani ili kuwawezesha kufanya kazi kwa usahihi, kwenda na wakati na kutumia teknolojia ya kisasa.

Msajili wa bodi hiyo, Albert Munuo amesema watawasaka wahitimu wanaofanya kazi bila kupitia mafunzo hayo. Pia, amesema mafunzo hayo yatawapa fursa wahitimu kujifunza kwa vitendo.

 

-->