Monday, July 8, 2013

Washindi wa Maonyesho ya Sabasaba watajwa

By Patricia Kimelemeta, Mwananchi

Dar es Salaam. Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshika nafasi ya kwanza kwa washindi wa jumla wa maonyesho ya 37 ya Mamlaka ya Kimataifa ya Biashara Tanzania(TanTrade).

Ushindi huo umekuja baada ya TanTrade kukagua mabanda yanayotoa huduma vizuri kwa wateja, jambo ambalo limewafanya washike nafasi ya kwanza.

Washindi wa pili katika maonyesho hayo ni pamoja ni Banda la Mamlaka ya Ukanda wa Uwekezaji Tanzania(EPZA) na washindi wa tatu ni Chuo Kikuu cha Ardhi.

Washindi wengine katika vigezo mbalimbali ni pamoja na Shirika la Viwanda vidogo vidogo(Sido),Kampuni ya Africa Tea Cofee, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL),Kiwanda cha Nguo cha Nida.

-->