MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa Rais Nkurunzinza aahidi kusimamia sera ya kilimo
BOOKMARK THIS PAGE
Rais Nkurunzinza aahidi kusimamia sera ya kilimo  Send to a friend
Wednesday, 20 April 2011 08:40

Boniface Meena
RAIS wa Burundi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afika Mashariki (EAC), Piere Nkurunzinza, ameitaka jumuiya hiyo kuwa na sera yenye nguvu ya kuboresha kilimo ili kuwa na uhakika wa chakula kwa nchi hizo.
Alitoa wito huo jana alipohutubia mkutano wa tisa wa viongozi wa EAC.

Nkurunzinza alisema sera bora ya kilimo itasaidia kukua kwa sekta hiyo na kupanua soko la mazao ya jumuiya kimataifa.

“Tunatakiwa kuboresha na kuongeza ujuzi katika kilimo ili kukuza soko letu la kimataifa,” alisema.

Katika mkutano huo viongozi wa EAC, walimteua Dk Richard Sizibera wa Rwanda kuwa Katibu Mkuu mpya wa jumuiya hiyo na Dk Enos Bukuku, kuwa Naibu katibu mkuu wake.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Sizibera alisema atasimamia sera za jumuiya hiyo na kuboresha soko la pamoja.

Sizibera alisema suala la ushuru wa pamoja nao ataendelea kuboresha na kusimamia jumuiya ya EAC kuwa bora zaidi.

“Nitaendeleza yale yaliyokuwa yamepangwa na katibu aliyemaliza muda wake na kuboresha mengine,” alisema.
Pia, alisema jumuiya itasimamia amani kwenye nchi zake na nyingine za Afrika ikiwamo Somalia.
Alisema kazi hizo atazifanya kwa kasi kama aliyokuwa nayo Balozi Mwapachu.

Hata hivyo, Sezibera alisema hajui ni changamoto atakazokutana nazo hadi atakapoanza kazi rasmi.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #2 2011-04-22 09:57
Kikowapi KILIMO KWANZA Tanzania?
Quote
 
 
+1 #1 2011-04-21 11:25
Jina la general secretary mpya wa EAC ni Sezibera, apana Sizibera. Asanteni
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner