MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa Kituo cha afya Nyamongo chakosa dawa ya malaria
BOOKMARK THIS PAGE
Kituo cha afya Nyamongo chakosa dawa ya malaria  Send to a friend
Tuesday, 19 October 2010 09:07

Anthony Mayunga, Tarime

KITUO cha Afya Nyamongo wilayani Tarime hakijapata dawa ya mseto inayotibu malaria  kwa kipindi cha miezi mitatu  hadi sasa.

Tatizo hilo linakwenda kinyume na kampeni za kupambana na malaria kwa kuwatibu wagonjwa ambayo inasisitiza kwamba Watanzania watapata vyandarua na dawa sahihi za kutibu malaria.

Uchunguzi wa  uliofanywa na Mwananchi katika kituo hicho  kilichoko katikati ya eneo la mgodi wa dhahabu wa North Mara ,ulibaini ukubwa wa tatizo hilo na wananchi kuonyesha kukata tamaa juu ya
mikakati inayonadiwa na viongozi kutokomeza malaria nchini. Marwa Ryoba mkazi wa Nyangoto alisema wanalazimika kutumia dawa za krolokwini,metakefilini na SP ambazo zilikwishapigwa marufuku na serikali kwa kushindwa kutibu ugonjwa huo.

“Tunashangaa ahadi na tambo nyingi za serikali kuwa watatokomeza malaria wakati hatupati dawa , hivi kupewa vyandarua na Wamarekani bila dawa inatusaidia?”alihoji kwa uchungu.

Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dk George Marwa alikiri kuwa hawajapata
dawa mseto licha ya kutoa taarifa  kwa zaidi ya miezi mitatu. “Hapa tunapambana na matatizo makubwa maana jamii haijui tatizo la Msd badala yake lawama zinaelekezwa kwetu,maana kama hakuna Alu unadhani huko wanatumia nini,”alisema. Kuhusu kadi za kiliniki hakuna na wajawazito na wenye watoto
wanalazimika kununua mitaani inadaiwa wananunua Sh2,000= maana hatuna,na hilo linawakatisha tamaa wasiokuwa na fedha kuhudhuria
kiliniki.
“Hapa tunahudumia zaidi ya watu laki moja kutoka kata zaidi ya nne za Tarime na Serengeti, glovu unapewa pc 50 kwa miezi mitatu ,wakati hizo ni kwa wiki  moja,wanalazimika kununua, na ni tatizo la mfumo.

Awali  mwanamke aliyekutwa katika kituo hicho akisubiri huduma jina tunao ,alisema kuwa wanachofanya ni kwenda kuandikiwa tu kisha wanakwenda kununua dawa kwenye maduka ya watu ambao pia si wataalam.
“Wengi tunatumia panadol wakati unaumwa malaria na hata kwa watoto
,matokeo yake panapotokea vifo inakuwa vigumu kujua nini tatizo ,maana wapo wanaoishiwa damu, lakini tunashindwa watibiwe na nini,”alisema.

Alikwenda mbali na kudai kuwa matatizo ya wananchi kwa huduma za afya yamegeuka kuwa mtaji kwa wanasiasa wanafiki,kwa kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki,”suala la dawa limeshindikana  sasa wanadai malaria
itakuwa historia kwa kuua ama nini?”alihoji kwa masikitiko.Baadhi ya wajawazito na wenye watoto waliokuwa hapo kituo
cha afya walisema mbali  na dawa ya malaria pia wanalazimika kununua kadi na glovu kwa kuwa hazipatikani hapo kituoni .


“Pembeni wanasema huduma kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano bure ,lakini hapa tunanunua dawa,mipira ya mikononi(Gloves)na kadi za kiliniki,wengi wanajifungulia majumbani na hawaleti watoto
kiliniki akiugua malaria wananunua panadol na dawa za kienyeji,”walisema.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #2 2010-10-20 07:50
Msimpigie kura huyu muheshimiwa sana Kikwete. Jamaa kamba tupu hana lolote jipya. Atasemaje kuhusu hili swala?
Quote
 
 
0 #1 2010-10-19 21:07
Duhh! haya hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania kwa miaka mitano iliyopita sasa tunaelekea kwenye ahadi nyingi kuliko hata zile za 2005. Viwanja vya ndege, ununuzi wa meli na ujenzi wa mabarabara ya lami kila mtaa na reli mpya kila mahali..... Mungu turehemu wanao!!!
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner