Thursday, December 7, 2017

Ecobank yaipa shule Dar maji safi na salama

 

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya

  Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Hananasifu, Idda Uisso, akimwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank baadhi ya mabomba ambayo kwa sasa yanatoa maji salama baada ya kufanyiwa ukarabati na benki hiyo 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha upatikanaji na usambazaji wa huduma ya maji safi na salama katika shuke ya msingi Hananasif wilayani Kinondoni.

Miundombinu hiyo hiyo itawezesha uopatikanaji wa maji katika vyoo na maeneo yenye uhitaji wa maji kwa  wanafunzi na waalimu wote.

Msaada huo umetoleewa kama sehemu ya maadhimisho siku ya Ecobank ambayo hufanyika kila mwaka katika nchi 33 barani  Afrika ambako Ecobank inafanya biashara.

Msaada huo umetolewa leo ikiwa njia moja wapo ya kuadhimisha   kauli mbiu ya mwaka  huu ya siku ya Ecobank inayosema   ‘Maji Salama, ishi na afya njema’.

Pamoja na msaada huo, wafanyakazi wa Ecobank Tanzania pia wamejumuika kufanya usafi wa mazingira shuleni hapo kwa kuzibua mitaro ya maji taka yote pamoja na kuweka dawa kwenye kisima cha maji shuleni hapo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama.

Kwa upande wa elimu, Ecobank pia  imetoa vitabu kwa wanafunzi wa  shule hiyo pamoja na kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi  waliofanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao kuanzia darasa la kwanza hadi la sita.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee, amesema benki hiyo imekuwa ikiadhimisha siku ya Ecobank kwa kutoa sehemu ya faida wanayopata kwa Jamii inayowazunguka.

 “Tuliguswa sana baada ya kupewa taarifa kuwa shule ya Hananasif ina jumla ya wanafunzi 728 lakini miundombinu ya maji imeziba na kubakia na sehemu moja tu  ambayo inatumiwa na shule nzima. Vyoo havina maji na hivyo imekuwa ni changamoto ya kiafya kwa wanafunzi, walimu na watu wengine kwenye shule hii, tukaona ni vyema kuja kusaidia ” alieleza Mwanahiba Mzee

Amesema kutokana na Benki yake kutoa msaada huo pamoja na vitabu vya kiada, motisha yaa zawadi kwa wanafunzi  itasaidia kutoa hamasa kwa wanafunzi kuendelea kuongeza bidii kwenye masomo yao zaidi

 “Ecobank Tanzania inatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora pamoja na kuboresha elimu ikiwa ni dhamira yetu katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu hapa nchini,” ameongeza.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Hananasif, Idda Uisso, ameishukuru benki hiyo kwa kuhakikisha shule hiyo inapata maji salama.

“Nachukua hii fursa kuwapongeza uongozi wa Ecobank Tanzania kuchagua kuja shule ya Hananasif kwani hapa kuna shule zingine nyingi,” amesema na kuongeza:

“Kwa msaada wa mamboresho ya miundombinu yote mliyofanya, kwa sasa tuna uhakika wa maji safi na salama kwa waalimu pamoja na wanafunzi” alisema.

 

 

-->