MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa DC ataka ushirikiano wa maendeleo kuimarishwa
BOOKMARK THIS PAGE
DC ataka ushirikiano wa maendeleo kuimarishwa  Send to a friend
Thursday, 19 May 2011 19:37

Kwirinus Mapunda, Mbinga
MKUU wa Wilaya ya Mbinga,  Edmound Mjengwa ametaka kuimarishwa kwa ushirikiano katika masuala ya maendeleo ya watu baina ya serikali na asasi zisizo za kiserikali ili kufikia malengo ya kupunguza umaskini nchini.

Mjengwa alitoa wito huo kwenye hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Habari cha Kijamii kilichojengwa katika Kijiji cha Maguu wilayani humu kwa msaada wa Marekani kupitia asasi isiyo ya kiserikali.

Alisema  kwa kawaida , serikali kazi yake ni kuhamasisha maendeleo kwa wananchi na kwamba malengo hayo yanaweza kufikiwa kama asasi nazo zitashirikiana vizuri kutekeleza majukumu yake.
“Serikali  kwa kushirikiana na asasi zote inaweza kufanikiwa vema katika kufikisha maendeleo vijijini na hatimaye kufikia malengo ya millennia.”, alisema.

Kituo cha Habari cha Jamii Maguu, kilijengwa kwa msaada wa Marekani na kwamba jengo lake lina vyumba vitano kikiwamo cha maktaba ambayo wananchi watakuwa wakikitumia kupata habari  mbalimbali kupitia vitabu na magazeti .

Awali,  mwenyekiti wa asasiiliyojenga kituo hicho, Christian Ndunguru akizungumza machache, alisema  lengo la kituo hicho ni kuhamasisaha wakazi vijijini wapate habari mbalimbali za dunia.Alisema kituo hicho kwa sasa kitakuwa na wafanyakazi watatu na kwamba kitapokea magazeti ya kila siku likiwamo Gazeti la Mwananchi.

Naye  mwakilishi wa wafadhili, Gregory Haman, alisema kituo hicho ni moja ya misaada ya kijamii ambayo inatakiwa kuwafikia wananchi.Alisema kwa kawaida wananchi wengi wanakosa habari jambo ambalo linatakiwa wasaidiwe kwa kujengewa vituo vya kupata habari mpya za kila siku.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #1 2011-05-24 12:27
Ni hatua nzuri ya kuwafikia watanzania wa vijijini na nashauri waongeze na kukipanua kituo kitoa habarin eneo la mwambao wa ziwa nyasa na maeneo jiran ya wilaya zinazopakana na mbinga
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner