
| ATCL hoi bin taabani: Serikali | Send to a friend |
| Tuesday, 02 August 2011 19:47 |
|
Katika swali lake, Kafulila alitaka kujua kuna ndege ngapi zinazofanya kazi na akahoji ni kwa nini kwa muda mrefu Tanzania inashindwa kuwa hata na ndege moja kama ilivyo kwa nchi ndogo kama Burundi.Awali, katika swali la msingi, Rukia Ahmed (Viti Maalum-CUF) alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kusafisha menejimenti pamoja na shirika hilo. Mbunge huyo pia alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kufufua Shirika la ndege la Tanzania kutokana na shirika hilo kuonekana kuelekea kufa.Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba alisema Serikali inatambua na kutafuta namna bora ya kulifufua shirika hilo ili liweze kuwa imara kama ambavyo Watanzania wanatarajia. Alisema kuwa Serikali iko katika mchakato wa kuteua menejimenti na bodi mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kusimamia Kampuni ya Ndege ya Tanzania ili iweze kufikia malengo. Naibu Waziri alisema kwa sasa Serikali inatarajia kuipatia kampuni vitendea kazi na mtaji wa kujiendesha ili iweze kuendeshwa kwa biashara bila ya kutegemea ruzuku kutoka serikalini.Alisema serikali iko mbioni kumpata mbia mahiri na mwenye uwezo wa kubadilisha ATCL iweze kutoa huduma za hali ya juu kwa ufanisi mkubwa sambamba na kampuni zingine nchini. Kwa mujibu wa Naibu Waziri, ndege iliyokuwa kwenye metengenezo nchini Afrika ya Kusini, inatarajia kurudi nchini Agosti 8 kwa kuwa sasa iko tayari kwa ajili ya kutoa huduma. |















Comments
NI MANENO KAMA HAYAHAYA MIMI NILIYASIKIA MWAKA JUZI, HIVYO HAWA CCM HUA SI WATEKELEZAJI WANACHEZA NA AKILI ZETU, WANACHOKIFANYA NI COPY AND PASTE ZA HUTUBA NA EDITING.
JAMANI JIULIZENI KWANI KUTEUA BODI HUA INACHUKUA MIEZI AU MIAKA MINGAPI WAKATI SERIKALI INAWAJUA WATU NA CV ZAO ZINAJULIKANA?