
| Kombani: Daraja la Kilombero litajengwa | Send to a friend |
| Thursday, 20 May 2010 19:03 |
|
SERIKALI imewahakikishia wananchi wa Wilaya za Ulanga na Kilombero, mkoani Morogoro, juu ya azma yake ya kukamilisha ujenzi wa daraja la Mto Kilombero, ndani ya kipindi kingine cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Celina Kombani, akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Ulanga Mashariki. Waziri huyo pia ni mbunge wa jimbo hilo. Kombani alisema katika kipindi cha muhula wa kwanza wa uongozi wa Rais Kikwete, serikali ilikuwa inakamilisha hatua za usanifu na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa daraja hilo. Alisema hatua hizo sasa zitafuatiwa na kuanza kwa ujenzi utakaofanyika ndani ya muhula wa pili wa serikali ya awamu ya nne. Kauli hiyo ilikuja baada ya baadhi ya wananchi wa Ulanga, kumuuliza waziri huyo kuhusu mpango wa serikali kujenga daraja la Mto Kilombero, ambalo Rais Kikwete aliahidi kulinega. Akiwajibu wananchi hao, Kombani alisema ujenzi wa daraja katika Mto Kilombero, uko katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kwamba lazima ufanyike. Alisema tayari serikali imeshatumia zaidi ya Sh 800 milioni kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa daraja hilo, likalomaliza kero ya wananchi wa wilaya hizo mbili, kuvuka katika mto huo mkubwa. Waziri Kombani alisema kwa sasa serikali iko katika mchakato wa mwisho wa kulitafutia fedha daraja hilo ili ujenzi wake uanze mapema iwezekanavyo. Aliwataka wananchi wa Wilaya za Ulanga na Kilombero, kuachana na baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaodai kuwa daraja hilo halitajengwa. |















Comments
Mdau wa kata ya Ruaha, mahenge.