MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa ‘Serikali, mashirika ziondoa kero kilimo na mifugo’
BOOKMARK THIS PAGE
‘Serikali, mashirika ziondoa kero kilimo na mifugo’  Send to a friend
Saturday, 28 January 2012 08:51

Esther Mwimbula ,Morogoro.
SERIKALI imetakiwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yanayojihusisha mifugo na kilimo ili waweze kuwasaidia kutatua kero mbalimbali zinazokabili sekta hiyo zilizodumu muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi hali iliyosababisha sekta hiyo kushindwa kutoa mchango mkubwa katika kusaidia kuleta maendeleo kwa jamii.

Hayo yalibainishwa kwenye mkutano ulioitishwa na wadau wa sekta ya nyama nyekundu uliandaliwa kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) kwaajili ya kujadili mafanikio na matatizo yanayoikabili sekta hiyo uliofanyika mkoani Morogoro.

 Mratibu  wa SNV, Silvanus Mruma  alisema kuwa  mfumo wa uingizaji wa chanjo nchini umekuwa ukisababisha kukosekana kwa chanjo za mifugo kirahisi hivyo kuiiasa Serikali kufanya utafiti  juu ya usimamizi na uendeshaji wa utoaji chanjo nchini ili kupata ufumbuzi wa  kero katika sekta hiyo inayoshikiliwa zaidi na wadau mbalimbali wa kilimo na ufugaji.

Mruma alisema kuwa  licha ya sekta hiyo kukumbwa na matatizo ya chanjo bado maofisa na wasimamizi wa sheria za mifugo wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kuingiliwa kiutendaji na wanasiasa hivyokushindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi akieleza kuwa wakati umefikia kwa maofisa hao kusimamia sheria kwa kuwajibike  kwa wizara ili wafanye kazi zao bila kuingiliana katika madaraka .

Alisema kuwa baada ya kero hiyo kugundulika  chama hicho kimeamua kuunda kikosi kazi kitakachoshirikiana na wadau mbalimbali wa nyama nyekundu kutatua kero hizo na kupata ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili sekta hiyo.
Alisema kuwa mkutano huo ulichagua kikosi kazi chenye wajumbe watano ambao kwa pamoja watahusika katika kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yatakayosaidia kuondoa kero zinazoimkumba sekta ya nyama nyekundu ikiwemo ya utoaji wa chanjo kwa wakati.

Mbali na hayo kikosi kazi hicho kutasaidia ujengwaji wa majosho kwaajili ya mifugo na utoaji wa pembejeo za mifugo kwa wakati hali aliyosema itasaidia kuimarisha sekta hiyo na kutoa mchango katika kujenga uchumi kikamilifu.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner