MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa Lions yatenga 100 mil kwa shule za Dar
BOOKMARK THIS PAGE
Lions yatenga 100 mil kwa shule za Dar  Send to a friend
Saturday, 28 January 2012 08:57

Fredy Azzah
KLABU ya Lions , imetangaza kutenga Sh100 milioni kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule za Dar es Salaam vifaa vya shule ikiwa ni pamoja na madaftari, kalamu na vitabu.

Mkuu wa Lions Club hiyo Tanzania na Uganda (District Governor) Satish Sharma, alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi baiskeli tano za walemavu kwa mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji na kuwagawia Wanafunzi wa Shule ya Msingi Gerezani ya jijini vifaa mbalimbali vya shule.

“Huu ni mwendelezo wa kusaidia jamii yetu ya Kitanzania,  vitu hivi tutavitoa kwa shule zote za Dar es Salaam,” alisema Sharma.

Alisema kuwa, lengo Lions Club ni kuhakikisha watoto kutoka jamii zote wanapata elimu bila kuwa na kipingamizi.
Alibainisha kuwa baiskeli walizotoa ni kwa ajili ya wananchi wa Singida Mjini ili waweze kufanya shughuli zao bila kipingamizi.

Kwa upande wake Dewji, aliishukuru klabu hiyo kwa msaada huo na kuwataka wafanyabiashara wengine kuwa kujifunza kurudisha faida kidogo wanayoipata kwa jamii.

“Siyo wafanyabiashara wote wanaweza kurudisha sehemu ya faida yao kwa jamii, nawashukuru sana Lions Club kwa hatua yao kubwa waliyoichukua, nawataka na wafanyabiashara wengine wawaige Lions Club,” alisema Dewj.
Alisema kuwa, ulemavu ni tatizo kubwa nchini ambalo kwa kiasi kikubwa linawafanya wananchi wengi kushindwa kutimiza majukumu yao.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner