MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa Mbunge ataka Serikali ifute kilimo cha tumbaku
BOOKMARK THIS PAGE
Mbunge ataka Serikali ifute kilimo cha tumbaku  Send to a friend
Saturday, 04 February 2012 08:39

MBUNGE wa wa Viti Maalumu Rukia Kassim Ahmed (CUF), ameihoji Serikali ni kwa nini inahamasisha kilimo cha tumbaku huku ikijua kuwa zao hilo ni hatari kwa watumiaji akiitaka ifute kilimo cha zao hilo.
 
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akiuliza swali la nyongeza katika kipindi cha maswali bungeni ambapo aliitaka Serikali ipige marufuku kabisa kilimo cha zao hilo na kisiwepo nchini.

“Kwa nini Serikali inahimiza kilimo cha tumbaku huku ikijua kuwa kilimo hicho ni hatari kwa maisha ya watu? Kitendo cha Serikali kuhimiza kilimo hicho ni kuchochea magonjwa ya saratani, shinikizo la damu na kisukari,’’alisema Rukia akihoji.

Awali katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini magonjwa ya Presha, kisukari, kansa na Moyo yanzidi kushika kasi nchini.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya alisema kuwa Serikali inahamasisha kilimo hicho kutokana na matumizi mbalimbali ya zao hilo lakini, si kwa uvutaji tumbaku tu.

Dk Nkya alisema tumbaku ni kati ya mazao yanayotumika kwa ajili ya kutengeneza dawa za kuua wadudu na kwamba kila anayetumia tumbaku anatakiwa kujua wazi kuwa anahatarisha afya yake.

Alidokeza kuwa ili kuondokana na lawama kwamba viwanda vinatengeneza sigara kwa ajili ya kupunguza nguvu kazi ya taifa, tayari Serikali imetoa maelekezo kwa kila kiwanda cha sigara kuweka nembo katika maganda ya sigara kuwa tumbaku ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

 Dk.Nkya alisema kuwa sababisho ya maradhi hayo ni pamoja na ukosefu wa lishe bora, matumizi ya utumiaji wa tumbaku pamoja na kutofanya mazoezi.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner