
| Familia 23,000 zafaidika na Pride | Send to a friend |
| Saturday, 04 February 2012 08:45 |
|
ZAIDI ya familia 23,000 nchini zimenufaika na mikopo ya fedha, mifugo na zana za kilimo zinazotolewa na shirika lisilokuwa la Kiserikali la Pride Tanzania lenye makao yake jijini Arusha na kuboresha maisha yao. Mkurugenzi Mtendaji wa Pride Tanzania, James Obama alisema hayo alipokuwa akielezea mafanikio na changamoto za mpango wa mikopo vijijini tangu uanzishwe mwaka 2007 . Obama alisema mwaka 2007 Pride Tanzania iliamua kuelekeza nguvu zake kwa wakulima vijijini ili kuwapatia mikopo hiyo ambayo huilipa wakati wa mavuno kwa nia ya kuwawezesha kuinua na kuboresha shughuli zao za uzalishaji mali . Alisema Pride ambayo imekuwa ikijihusisha na utoaji wa fedha kwa wajasiriamali tayari imeshatoa mikopo ya mifugo kupitia vikundi vya wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambako Shirika la Pride Tanzania limewapa mikopo ya ng'ombe wa kisasa na sasa wanazalisha maziwa mengi ambayo wanayauza viwandani. Alisema Pride Tanzania, mwaka 2007 ilipanua shughuli zake za utoaji mikopo kwa awamu, ambapo awamu nyingine ya mikopo ya zana za kilimo ilianza kutekelezwa mwaka 2009 wilayani Kilolo huko Iringa. Aliongeza kuwa, baada ya mafanikio kupatikana Pride ilipanua huduma zake za utoaji mikopo ya zana za kilimo katika Wilaya za Kilosa, Morogoro vijijini na Mvomero mkoani Morogoro, ambapo wakulima katika wilaya hizo wamenufaika na mikopo hiyo. |














