MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa Tanga Cement yatoa msaada
BOOKMARK THIS PAGE
Tanga Cement yatoa msaada  Send to a friend
Tuesday, 10 August 2010 20:52

Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Tanga Cement imekabidhi msaada wa darasa pamoja na samani zake zenye thamani ya Sh 20.6 milioni kwa Shule ya Sekondari ya Mruwia, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo juzi shuleni hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Erik Westerbeg alisema ujenzi wa darasa hilo umepitia katika mpango wa kuwekeza katika jamii na kwamba kampuni yake ina inaweka mkazo katika maeneo ya afya, elimu na maendeleo ya jamii na mazingira.

Alisema katika maeneo hayo, elimu imepewa kipaumbele ikiwa ni juhudi za  kuingua mkono serikali katika jitihada zake za kuboresha elimu nchini.

“Unapoelimisha jamii mambo mengine yanawezekana kwa urahisi, mtu aliyeelimika anaweza kutunza mazingira, kutunza afya yake na pia kuchangia maendeleo ya jamii,” alisema.

Alitoa wito kwa uongozi wa shule hiyo na wanafunzi  kuongeza juhudi ili shule hiyo ifanye vizuri  kwa lengo la kuwavutia wahisani wengine.

Awali akisoma risala ya shule hiyo, Mkuu wa shule hiyo, Faustine Temba aliishukuru kampuni hiyo na alisema shule hiyo, inakabiliwa na matatizo, yakiwemo  ukosefu wa vyumba vya madarasa, vitabu na walimu.

Mkuu huyo alisema shule yake iliyoanza kujengwa mwaka 2007 kwa sasa ina  wanafunzi 366 wa kidato cha kwanza hadi cha nne, wavulana 188 na wasichana 178 na ina walimu wanne tu walioajiriwa na serikali.

“Walimu hawatoshi, tuna vyumba 11, lakini madarasa 10 kati ya hayo, yanatumika yakiwa hayajakamilika hivyo tunaishukuru Tanga Cement kwa kutupa darasa lililokamilika likiwa na samani zake,” alisema.

Mkuu huyo alimshukuru pia Mbunge aliyemaliza muda wake wa Moshi Vijijini, Dk Cyril Chami kwani alisema juhudi zake zimechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa msaada huo.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner