MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa Sumatra yapata Sh 14 milioni kwa madereva wazembe
BOOKMARK THIS PAGE
Sumatra yapata Sh 14 milioni kwa madereva wazembe  Send to a friend
Thursday, 02 September 2010 22:11

Agatha Mboya, Mbeya
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Kanda Nyanda za Juu Kusini  imepata Sh 14 milioni za faini kutokana na makosa mbalimbali ya madereva wanaokiuka taratibu.
 
Mkurugenzi wa Sumatra kanda hiyo,  Amani Shamaje alisema fedha hizo zilikusanywa katika kipindi cha mwezi wa Mei  mwaka huu pekee katika operesheni iliyofanyika mkoani Mbeya kuwabana madereva wanaokiuka taratibu za usafirishaji”.
 
Shamaje alisema katika operesheni hiyo magari zaidi ya  50 yalikutwa na makosa ya uvunjaji wa sheria za usafirishaji na kwamba faini kwa kila gari ilikuwa  Sh 250,000.

Akizungumzia kuendelea kwa operesheni hiyo, alisema katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi wa madiwani, wabunge na Urais, Sumatra kanda hiyo imeamua kusitisha kazi hiyo kutokana polisi kujikita zaidi katika kusimamia suala la usalama wa wagombea hao na wananchi.

 “Ni suala la ustaarabu tu, huwezi ukaanza kuwakamata madereva wanaovunja sheria hizo na hasa ukizingatia  uchaguzi mkuu unagusa maisha ya watu, hivyo ili kuepusha vurugu zisizo na msingi ni vema tukaacha mpaka mwezi Novemba mwaka huu, mambo ya uchaguzi yatakapokuwa yamekwisha” alisema.
 
Hata hivyo alitoa wito kwa madereva kuacha mra moja kuvunja sheria za barabarani na kwamba  wavunjaji watachukuliwa hatua  za mara moja watakapobainika.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner