MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa TLTC yatoa Sh118 mil kusaidia jamii Urambo
BOOKMARK THIS PAGE
TLTC yatoa Sh118 mil kusaidia jamii Urambo  Send to a friend
Thursday, 02 September 2010 22:16

Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Ununuzi wa Tumbaku Tanzaia (TLTC), imeukabidhi uongozi wa serikali wilayani Urambo,Sh118.2 milioni, ili zitumike katika shughuli za jamii.

 Hundi ya fedha hizo ilikabidhiwa juzi kwa Mkuu wa wilaya hiyo, Anna Magoha, katika hafla fupi iliyofanyika katia ukumbi wa Maria, mjini Urambo.
Ilikabidhiwa na Meneja Mkuu wa Shughuli katika TLTC, Kanda ya Magharibi, Thadeo Lyimo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi hiyo, Lyimo alisema pamoja na kununua tumbaku, inayolimwa wilayani Urambo, kampuni yake imekuwa ikisaidia jamii ya watu wa wilaya hiyo.

Alisema mchango wa kampuni yake kwa watu wa Urambo, unaelekezwa zaidi katika maeneo ya  elimu, maji na afya, ukiwa ni mkakati wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuharakisha maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo ya Mkoa wa Tabora.

Alifafanua kuwa fedha hizo zitatumika katika kuboresha sekta ya elimu kwa kujengea nyumba za walimu, vyumba vya madarasa, mabweni na vyoo vya kisasa.

"Lakini pia sehemu ya msaada huu itasaidia katika ujenzi wa ofisi za serikali kwenye kata na visima vya maji ambavyo siyo tu vitasaidia wanafunzi na walimu mashuleni, lakini pia wananchi kwa jumla," alisema Lyimo.

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya hiyo (, aliishukuru TLTC kwa msaada huo ambao alisema ni wa muhimu katika maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo. Magoha alizisihi kampuni nyingine zinazonunua tumbaku katika Wilaya ya Urambo, kuiga mfano wa TLTC.

“Msaada huu ni ishara kwamba ninyi ni wadau wetu halisi wa maendeleo, kwani siyo tu kwamba mnaunga mkono kauli mbiu ya serikali ya Kilimo Kwanza, lakini pia mnajali maisha ya wananchi wa wilaya ya Urambo,” alisema

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner