MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kitaifa Watanzania washauriwa kuacha uvivu
BOOKMARK THIS PAGE
Watanzania washauriwa kuacha uvivu  Send to a friend
Tuesday, 01 March 2011 19:50

Venance George, Morogoro



MKUU wa zamani wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga, amesema umasiki wa Tanzania hauwezi kumalizika kama watu wake, hawataacha uvivuna kukataa kuongeza bidii katika kufanya kazi.



Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari  wa Taasisi za Kikristo Tanzania lililofanyika juzi mjini Morogoro, Mashishanga alisema, umasikini ndiyo kiini cha machafuko katika nchi nyingi za dunia.

Alisema kwa kuzingatia hilo, kuna haja kwa Watanzania, kujipanga na kufanyakazi kwa bidii, ili kuondokana na umasikini.

"Ukichunguza migogoro mingi iliyoko katika mataifa mbalimbali duniani, utabaini kuwa mingi inachochewa na umasikini na hii pia iko katika ngazi ya familia," alisema mkuu huyo wa zamani wa mkoa.

Alisema familia inayokabiliwa na  umasikini, lazima itakuwa na migogoro ya mara kwa mara na hatimaye, kukosa amani.

Alisema dawa pekee ya kuondokana na hali hiyo, ni watu kuondokana na uvivu na kufanya kazi kwa bidii.

Mashishanga, alielezea matumaini yake kuwa kufanya hivyo kutaiwezesha Tanzania kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo mwaka 2025.

Mashishanga pia aliwataka waandishi kuzitumia vema kalamu zao kwa kuandika mambo yatakayoliwezesha taifa, kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

"Ikiwa waandishi wa habari wa taasisi za Kikristo  mtazitumia vizuri kalamu zenu mtakuwa katika nafasi ya kujitofautisha na waandishi wa habari wengine wanaoandika mambo bila kuzingatia maadili na kusababisha magomvi mengi," alisema. 

Kongamano hilo liliwajumuisha waandishi wa habari wa Taasisi za Kikristo kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Pamoja na waandishi hao, pia lilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Mradi wa vyombo vya habari kutoka Marekani, Mchungaji Dk Arne Fjeldestad.

Kwa upande wake mkurugenzi huyo alisema mradi huo umeanzishwa ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari wakristo duniani, kutumia vizuri taaluma yao.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner