MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kimataifa Maandamano yavunja mazungumzo ya uchumi Ulaya
BOOKMARK THIS PAGE
Maandamano yavunja mazungumzo ya uchumi Ulaya  Send to a friend
Monday, 19 September 2011 08:46

VIROSLAV,Poland
WAKATI Mawaziri wa Fedha wa Nchi zinazotumia sarafu ya Euro walipokutana mjini Virostlav ,nchini Poland watu zaidi ya 40,000 wamevamia mazungumzo ya mzozo wa uchumi.

Waandamanaji hao eneo lililokuwa linatumiwa na mawaziri hao wa fedha kwa lengo la kupinga mazungumzo hayo,ambayo yalikuwa yakiongozwa na Rais wa kundi  la  Mataifa  hayo  Jean Claude Juncker.

Mawaziri  wa Fedha wa Nchi zinazoitumia sarafu ya euro walikutana mjini Virostlav nchini Poland kwa mazungumzo ya siku mbili kuhusu mzozo wa madeni katika nchi zao.

Kutokana na kiasi cha waandamanaji 40,000 wanaopinga hatua za kubana matumizi walikwamisha shughuli katika mji huo hapo juzi.

Mazungumzo hayo yalilazimika kumalizika mapema kutokana na maandamano hayo licha ya kuwa na ulinzi wa kutosha.

Pia katika kikao hicho mawaziri hao wa fedha waliamua kuahirisha uamuzi kuhusu uwezekano wa mkopo wa pili kwa Ugiriki hadi mwezi Oktoba.
 
Rais wa kundi  la  Mataifa  hayo  Jean Claude Juncker alisema Umoja wa Ulaya na shirika la fedha la kimatiafa IMF zinahitaji kuona mageuzi yakiendelezwa nchini Ugiriki kabla ya kutolewa awamu nyingine ya mkopo.

Wakati huo huo waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner ambaye alihudhuria mazungumzo hayo, aliziomba nchi zinazotumia sarafu ya euro kuendeleza mipango  itakayoinua  uchumi wa nchi hizo badala ya kuangalia sana tatizo la matumizi ya serikali.

Mawaziri hao  walipinga vikali matamshi hayo na kuiambia Marekani kutatua matatizo yake.
Wakati huo huo waziri wa fedha wa Ujerumani kwa mara nyingine tena alitoa wito wa kutozwa kodi kwa biashara za fedha miongoni mwa nchi 17 zinazotumia sarafu ya euro.

Wolfgang Schauble aliliambia gazeti la kila  jumapili nchini Ujerumani la  Bild am Sontag kuwa kodi hiyo itapangwa baadaye mwaka huu licha ya  upinzani  mkali kutoka mataifa kama vile Marekani na Uingereza.

Waziri mwenzake wa Ubelgiji, Didier Reynders alimuunga mkono akisema kuwa kodi hiyo inahitajika kuyatuliza masoko.

Waungaji mkono hatua hiyo kama vile nchi za  Ujerumani, na Ufaransa zinaamini kuwa kodi hiyo itasitisha ulanguzi,na kusaidia kupatikana fedha zitakazoweza kutumika kutoa mikopo kwa mabenki katika wakati  wa mizozo katika siku zinazokuja.

Wapinzani wanalalamika kuwa kodi ya aina hiyo itahamishia biashara kwenye masoko ya nchi ambazo hazitozi kodi


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner