MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kimataifa Obama atenga mabiioni kutaka mashoga watambuliwe
BOOKMARK THIS PAGE
Obama atenga mabiioni kutaka mashoga watambuliwe  Send to a friend
Wednesday, 07 December 2011 20:17

Mwandishi Wetu
MAREKANI imeungana na Uingereza kushinikiza kutambuliwa kwa haki za mashoga, ikitumia rungu la misaada yake inayotoa kwa nchi mbalimbali duniani, huku ikitenga Dola za Marekani 3 milioni sawa na Sh5.1bilioni, kwa ajili ya kufanikisha mkakati huo.

Shinikizo hilo la Marekani ambalo ni taifa kubwa kiuchumi duniani, linazidi kuchochea mjadala ulioibuliwa na  Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ambaye alitangaza katika mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uswis hivi karibuni kwamba,  nchi yake itasitisha misaada kwa nchi zote duniani ambazo hazitambui haki za mashoga.

Baada ya Cameron, Rais Barack Obama wa Marekani naye juzi alitangaza kwamba, taifa hilo kubwa litatumia uwezo wake wote ikiwamo misaada inayotoa kwa nchi mbalimbali kuhakikisha haki za mashoga zinatambuliwa na kuthaminiwa duniani.

Rais Obama alitoa msimamo huo jijini Washington katika hafla ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo , Hillary Clinton ambaye ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu.

“Wengine wanasema kuwa haki za mashoga na haki za binaadamu ni vitu tofauti na havifanani, lakini ukweli ni kwamba ni kitu kimoja na chenye usawa,”alisema Clinton wakati akisoma taarifa hiyo maalumu yenye baraka za Obama.

Clinton alisema, “Tayari tumetenga kiasi cha Dola za Marekani 3 Milioni kwa ajili ya programu ya kutangaza haki za mashoga ili kuondokana na ubaguzi na unyanyasaji dhidi yao.”

Waziri huyo wa mambo ya nje, alisema  mpango huo unazitaka nchi ambazo sheria zake bado hazitambui haki za mashoga na kubadilisha sheria hizo ili jamii hiyo ya watu ianze kutambulika.

“Kwa nchi ambazo watu wanafungwa, kupigwa kutokana na kuwa mashoga ni muhimu viongozi wa nchi hizo, kuangalia jinsi gani wanaweza kukiangalia kikundi hicho cha watu. Si kwamba mashoga hawafanyi makosa, wanaweza kufanya au kutokufanya kama watu wa kawaida, lakini isiwe ni kosa la jinai mtu kuwa shoga,”alisema.
Kwa mujibu wa Clinton, haki za mashoga ni haki za kimataifa. "Hazina tofauti na haki za binadamu zilizotambuliwa na nchi 48 lililotolewa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Naibu Msemaji wa Baraza la Usalama la Marekani, Caitlin Hayden alisema Serikali ya nchi hiyo si kwamba itapunguza au kuzuia misaada yake ya kimataifa ili kubadilisha utamadini wa nchi nyingine, bali inataka kuhakikisha haki za mashoga zinapewa pia kipaumbele.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Obama kujitokeza hadharani na kutetea haki za mashoga, lakini aliwahi kupitisha sera iitwayo “ don’t ask, don’t tell” ikimaanisha “usiulize, usiseme” ambayo inawazuia mashoga kujiunga na kufanya kazi za jeshi kwa uwazi.

Mmoja wa viongozi wa Republican ambaye atawania nafasi ya Urais, Gavana Rick Perry alisema Obama kwa mara nyingine amewakosea Wamarekani kwa aina tofauti ya maisha yao kwa kuingiza aina hiyo ya maisha kitu ambacho mtu kama yeye Perry hawezi kukifanya.

Kauli hiyo ya viongozi wa Marekani inaonekana kuungana na ile iliyotolewa na  Cameron aliyesema, "Hii ni moja ya vitu vinavyoongoza sera yetu ya misaada kwa mataifa mbalimbali na tayari tumeanza kuitekeleza katika maeneo kadhaa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #63 Faustin Mlelwa 2012-05-21 12:39
Watanzania tubaki na hamu ile ya kuishi na jinsia tofauti. Tukiingia kwenye hamu ya kuishi jinsia moja, ku wapi kutimiza agizo la Mungu la kuijaza dunia. Jinsia moja haiwezi kuleta mazao.
Quote
 
 
0 #62 Martine 2012-05-14 13:26
Tukiwa na chakula cha kutosha wala hatuhitaji misaada,kwani ukiwa na njaa ndio utahitaji msaada na hiyo inaweza kusababisha ukaingia kwenye mambo machafu,pole saana obama
Quote
 
 
0 #61 2012-03-20 02:25
NENO LINASEMA"KAMA WALIVYOKATAA KUWA NA MUNGU KATIKA FAHAMU ZAO,AKILI ZAO,MUNGU AKAWAACHA WAFANYE YASIYO WAPASA.HII INAONESHA KUWA HAWA VIONGOZI KATIKA AKILI ZAO WAMEMKATAA MUNGU,MTU YEYOTE MWENYE HOFU YA MUNGU HAWEZI KUTOA TAMKO KAMA HILI.HII INAASHIRIA KUWA AKILI ZAO NI CHAFU,MIOYO YAO IMEFURIKA MAOVU.NA KAMWE WATANZANIA HATUTAKUBALI HILI,NI BORA KUFA MASKINI KULIKO KUKUBALI U[NENO BAYA].NDIO MAANA WANAKUMBWA NA MAJANGA MAKUBWA KWA SABABU YA MATENDO YAO MACHAFU.WASHINDWE KWA JINA LA YESU.
Quote
 
 
+1 #60 2012-02-07 10:24
Hey people don't be fool! haya mambo yame andikwa ktk "BIBLE". kitabu cha UFUNUO chote, and last day events. Na 'MNYAMA' ataitawala Dunia ( AMERICA) Ata implementing [NEW WORLD ORDER] ktk Dunia! Na mambo yaliyomo ktk hiyo "ORDER" Moja wapo ni kuweka Sheria ya kumpinga KRISTO. Yapo mambo mengi ktk hiyo 'NEW WORLD ORDER'Kama "WATU KUABUDU SIKU MOJA KOTE DUNIANI". Kwa TUNAO AMINI kuwa MUNGU yupo na alijua kuwa DUNIA itakuwa na MA[NENO BAYA] lkn Akaweka AMRI/ {KARIPIO}! ULE WAKE AFIRWAYE/AFIRAE kwa KUWA' HATA URITHI UFALME WA MBIGUNI.BINADAMU Tusi mrekebishe MUNGU kwa ni'NI MWANZO NA MWISHO. GET HARD PRAYERS FOR THIS SIN! NI NGUVU KATI YA WANAO AMINI JUU YA MAMBO YA MUNGU NA WASIO AMINA JUU YA MAMBO YA MUNGU. mimi na AMINI JUU YA MAMBO YA MUNGU, JEE! WEWE JE? OMBA SANA RAFIKI
Quote
 
 
+1 #59 2012-01-17 13:29
Enyi watu wote wenye imani na kuyaamini maandiko matakatifu yasemayo;Na alaniwe afiraye na afirwaye,sasa ni wakati wa kumlilia Mungu ili atuepushe na balaa hili na tukumbuke kuwa siku zilzo tabiriwa na manabii ndo hizi,Ee Baba tusaidie si wanawo
Quote
 
 
0 #58 2012-01-16 15:14
yani huyo jamaa asituletee ufethuli
watakao pitisha hiyo sheria tutaanza kuoza familiazao
Quote
 
 
0 #57 2012-01-05 13:26
SASA KUNA KILA DALILI KWAMBA DINI HII YETU YA KIKRISTO INACHAKACHULIWA AU ILICHAKACHULIWA . SASA SISI MIMI NITAKUWA SINA DINI AU NITAAMIA ISLAM KAMA MAMBO YENYEWE NDIO HAYA.
Quote
 
 
0 #56 2011-12-23 04:34
Kwako tumaini.
Mi nilifikiri tumaini una akili. Najua sehemu ya akili zako zilipo kuna maji. Na sehemu ya maji ndipo kuna akili. Acha kutetea mambo ya ki[NENO BAYA] au na wewe unataka kuolewa?
Quote
 
 
0 #55 2011-12-23 04:30
Tusishangae tutakapo sikia David C. na Obama wanatangaza kuwa nao wanataka kuolewa.
Quote
 
 
-1 #54 2011-12-13 03:15
dad tumaini nakupongeza kwa msimao wako kuandika hapa inajua watanzania wengii wanajifanya wacha mungu na nini nini wameenda huko marekani wakaelwewa kwa nini obam anafanya hivyo?? Ya kwetu yanatushinda twayashupalia ya wamerikani mbona watu wanatafutadawa za mapenzi biashaara mivuto ya kazi sasa hao hawakiku ya mungu?? Tuacheni ushabiki wa mambo na wala hao ndugu zake wa kenya hawahusiniki na mfumo wa utawala wa kimarekani msichanganye ma[NENO BAYA]o!!!
Quote
 
 
+1 #53 2011-12-11 16:41
jamani tuanze kukirejesha kizazi cha mungu muumba wa mbingu na nchi.tuzifutilie mbali massmedia zao,biashara zao,tamaduni zao.mwisho tutafute rafiki mwema mcha mungu!nadhani mchina anafaa!kwani nyerere sio [NENO BAYA] kujihusisha nae aliyatambua haya.hebu oneni tunauzwa mpaka wanaume.wamewatamani dada zetu,wamewasher atisha sasa mpaka wanaume wanatutamani!ee h mwenyezi mungu wasamehe,ila ahadi za adhabu ya kuanguka kwao usiifute.waangushe wasije wakawaangusha wa fuasi wako.


~mwana jukwa naanza kukataa mimi massmedia zao.nakujifunza maandiko na elimu ya kweli walio zifuta za mungu wa kweli.

~nenda kwenye ovi store.tafuta biNu bible.ina kuruani ndani.kwa tafsiri zote.ina edition za bilia zote na tafsiri zote.ina wikipedia ya kweli,unaweza share idea hata kwa sms,email na ni bure!

~jamani tukirudishe kizazi cha mungu!chenye hofu ya mungu!
Quote
 
 
-1 #52 2011-12-11 16:22
Quoting tumaini nusurupia:
iNATAKIWA TUJIULIZE KWANZA KWA NINI MTU ANAKUA [NENO BAYA] ?
[NENO BAYA] INA SABABU YA MAMBO MBALI MBALI KIUTAALAMU.
HORMONES ISSUES, CHILDHOOD EXPERIENCES AND ASS ANATOMY WHICH MAY LEAD TO ADDICTION.
JEE UKIZAA MTOTO ANA KIFAFA, ALBINO AU KILEMA UTAMTENGA.
HAWA NI BINADAMU NA WANAHITAJI HESHIMA KAMA BINADAMU YEYOTE, ISITOSHE PIA LAZIMA TUHESHIMU MAAMUZI YA MTU VILE AMBAVYO ANAPENDA AWE.
WATANZANIA ELIMISHENI JAMII KWA AJILI YA BETTER FUTURE, TUSIENDEKEZE MISIKITI NA MAKANISA AMBAYO NI MFUMO WA KALE WA MAISHA.
WALIOLETA DINI AFRIKA WENYEWE WAMESHASAHAU DINI.
NAOMBA TUACHANE NA NDOTO ZA NDARIA.
TAFADHALI FUATENI KAULI ZA WENYE KUONA MBELE KWA SABABU WAO NDIO WAVUMBUZI NA WAENDESHAJI WA ELIMU.
JIULIZE NA MVUA ZOTE BADO UNAAGIZA MCHELE KUTOKA NJE, SEMBUSE KIBIRITI MPAKA LEO HUWEZI KUTENGENEZA.
TUWAHESHIMU MA[NENO BAYA] NI WATU KAMA MTU MWENGINE YEYOTE TUACHANE NA MILA ZA KALE.

(kwako tumaini!)

~laiti ungelifundishwa uelewe,ila vitabu vilivyo paswa kukufundisha vimefichwa.ila kwakuwa elimu yako niyajana,umekar irishwa ya jana tu.nawe ukatika angamio lao,na kizazi chako.think of a different between nature and nurture.dont talk to albinos nature of god creation to your shameless,meani ngless,sinfull nurture!
Quote
 
 
0 #51 2011-12-11 16:08
hapa naona uchu wa madaraka tuu!mtu huyu huyu aliwahi kutoa kauli ya kumsifu martine luther king siku chache zilizopita!kwa maadili ya kimungu.pili ni chachu ya kuishinikiza nchi maskini za afrika kuingia katika maadili machafu.ila kwa dhana na shinikizo la raia,iliasiachi e kiti imebidi nae kuwauza ndugu zake kama kahaba [NENO BAYA],akijisaha u kwamba kauli yake inamuambatanish a bibi,babu na ndugu zake huko kenya.ila ni tabiri za manabii zimatimia!
Quote
 
 
+2 #50 2011-12-09 10:11
this is definitely the end of U|SA
U think u are doing intimidation to the weak nations but actually u are finishing up yourself u american...
who will stand among u, where will uer position be on this universe?
Its GOD himself who will fight u and exterminate U Completeley u are CURSED!!!!!
U are Cursed forever,
Pit to your offsprings u weak NATION...
Let GOD Punish u accordingly and exterminate u sooner than uer Black plans!!!!!!!!!! !!!!
Quote
 
 
+1 #49 2011-12-09 09:24
Ndo hao hao descendents ya waliokataa taurat ya musa, zaburi ya nabii daudi, na injili ya nabii Mussa na QUR-AN ya Muhammad(S.A.W). wakabadilisha maneno ya M/mungu na wakatunga Biblia na dini ya UKRISTO. LKN WAJUE KWAMBA M/MUNGU YUPO SERIOUS ON THE PURPOSE OF CREATION; IS JUST A MATTER OF TIME WATALIA NA KUSAGA MENO NDANI YA MOTO WA JAHANNAMU
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner