Airtel yatoa punguzo la bei kwa bidhaa zake

Meneja wa huduma kwa wateja Bi Celine Njuju akionesha simu na vifaa vilivyopunguzwa bei katika maduka yote ya Airtel nchini. Kulia ni Meneja mauzo wa bidhaa za mawasiliano Airtel Pascal Maziku. Ofa ya simu na vifaa hivyo vya mawasiliano pia inaambatana na ofa ya dakika za muda wa maongezi pamoja, bando la intaneti na SMS bila kikomo kwa miezi sita

Muktasari:

  • Modern, simu za aina mbalimbali zahusika
  • Haya yamesemwa na Meneja wa Huduma kwa wateja wa kampuni hiyo, Celina Njuju, ambaye amethibitisha kuwa bidhaa hizo zinapatikana kwenye maduka yote ya Airtel.

Sasa hakuna haja ya Mtanzania kuhangaika na bidhaa za simu za mkononi zisizo na ubora kwani kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeshusha bei ya bidhaa nyingi ili kuwawezesha watanzania kuzipata kwa urahisi.

Haya yamesemwa na Meneja wa Huduma kwa wateja wa kampuni hiyo, Celina Njuju, ambaye amethibitisha kuwa bidhaa hizo zinapatikana kwenye maduka yote ya Airtel.

“Tunataka wateja wafaidi fedha zao. Siku zimepita ambapo Watanzania walikuwa wanaenda madukani na kununua bidhaa feki kwani kwa sasa tunazo bidhaa halisi kabisa ambazo zinapatikana kwa bei nafuu, alisema Njuju.

Baadhi ya bidhaa ambazo Airtel imepunguza bei ni Wingle USB Modem, simu za mkononi za aina mbalimbali.

Pamoja na bidhaa hizo, mteja atakayenunua pia atapatiwa bonsai inayohusisha vifurushi vya internet, ujumbe mfupi wa maandishi na dakika za bure za muda wa maongezi.

“Natoa wito kwa wateja wa Airtel kujitokeza na kufaidika na punguzo la bei ya bidhaa hizi kwenye maduka yote ya Airtel nchi nzima,” alisema Njuju.