BancABC yaja na akaunti mpya isiyo na gharama

Meneja wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa BancABC, Joyce Malai (kulia) na  Meneja Masoko wa benki hiyo, Upendo Nkini wakionyesha bango la  uzinduzi wa akauti mpya ya Hundi ya Jiongeze isiyo na makato ya mwisho wa jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

Lengo ni kufikia Watanzania wengi waweze kuwa na akaunti za hundi kwa bei nafuu.

 BancABC imezindua akaunti iitwayo Jiongeze Hundi inayolenga kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiriamali kufanya miamala bila kutumia gharama kubwa.

Akaunti hiyo inapunguza makato ya huduma za uendeshaji wa akaunti ya kila mwezi kwa wateja watakaoifungua.

Meneja wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Joyce Malai amesema akaunti ya Jiongeze inaweza kuwa ya biashara au ya mshahara lakini haitakatwa gharama kubwa za mwezi kwa muda wa mwaka mmoja tangu ifunguliwe.

“Faida zingine kwa wateja wa Jiongeze ni kuangalia salio sehemu yoyote kupitia simu ya mkononi, kuweka na kutoa fedha kupitia zaidi ya mawakala 50 ambao wanapatikana sehemu mbalimbali za Dar es Salaam, kupitia mtandaoni na ATM zenye nembo ya visa, pia kupitia aplikesheni ya BancABC,” amesema Malai.

BancABC mwaka huu imeshinda tuzo ya benki inayokua kwa haraka.

"Ubunifu na huduma zetu ndiyo unafanya BancABC kuwa tofauti Tanzania. Tumeelekeza nguvu katika kukuza na kuongeza matawi ili kila Mtanzania aweze kufikiwa na huduma za kibenki,” amesema Mkuu wa Masoko wa BancABC, Upendo Nkini.

Amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali kufungua akaunti ya Hundi ya Jiongeze kwa kuwa huduma hiyo itadumu kwa miezi miwili pekee.