CBA yaongeza mtaji kuboresha huduma

Muktasari:

  • Akizungumza na wateja wa benki hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita, mtendaji mkuu wa CBA, Dk Gift Shoko alisema mtaji wa zaidi ya Dola 2 bilioni walionao unawaweka miongoni mwa taasisi imara za fedha nchini.

Licha ya kupata hasara ya zaidi ya Dola 7.1 milioni za Marekani (zaidi ya Sh15 bilioni) mwaka 2017, Benki ya CBA imesema ipo imara kimtaji, huduma na utendaji.

Akizungumza na wateja wa benki hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita, mtendaji mkuu wa CBA, Dk Gift Shoko alisema mtaji wa zaidi ya Dola 2 bilioni walionao unawaweka miongoni mwa taasisi imara za fedha nchini.

“Wanahisa wameongeza zaidi ya Dola 7 milioni (zaidi ya Sh15 bilioni) kufidia madeni yasiyolipika,” alisema Dk Shoko.

Alisema benki hiyo haikabiliwi na tishio la kufungwa kutokana na kuwa na mtaji wa kutosha, utaalamu na mipango endelevu ya biashara.

“Kati ya Januari na Machi tumetoa mikopo ya zaidi ya Sh10 bilioni kwa wateja wa M-Pawa. Benki itaendelea kuwekeza kwenye teknolojia ili kuongeza ufanisi. Matumizi ya teknolojia hayakwepeki,” alisema Dk Shoko.

(Sada Amir)