Jinsi ya Kushughulika na Afisa Uajiri Msumbufu I BrighterMonday

Muktasari:

Umeshawahi kujiuliza ni jinsi gani unaweza kufaulu usaili wa kazi pale ambapo afisa uajiri ni msumbufu. Dondoo hizi zitakuwezesha kufaulu usaili huo.

Una mahojiano muhimu ya kazi umeyapanga. Umejiandaa, unajua taarifa zote za muhimu za kampuni. Katika ulimwengu usio na makosa, afisa uajiri wote ni watu wazuri. Lakini kawaida haipo hivvyo. Unaweza kupata afisa uajiri ambaye ni msumbufu au ni ngumu kumvutia.  Afisa uajiri anaetaka utimize sifa ambazo ni ngumu kuwa nazo. Anakuhoji kwa muda mrefu kiasi kwamba inakuwa ngumu kuonyesha ujuzi wako wa kazi. Usikate tamaa, BrighterMonday Tanzania tume orodhesha baadhi ya dondoo zitakazo kusaidia kufaulu usaili huo.

Usikubali Kudhalilishwa

Hata kama umekata tamaa kwenye mahojiano, usionyeshe hivyo. Elekeza umakini wako wote kwenye mahojiano. Badilisha kila swali katika fursa ya kuonyesha ujuzi wako. Sisitiza uwezo wako na mafanikio uliyopata. Unaweza kuona kuwa unaonewa lakini pengine kila mwombaji wa kazi alipitia utaratibu huohuo. Jizuie kuanza kujitetea, jibu maswali yote kwa mtazamo mzuri.

 

Mheshimu Afisa Uajiri

Hata unapohisi umeonewa, mheshimu afisa uajiri.Stay positive despite how difficult it may be. Tabasamu na tumia sauti tulivu, hii itaonyesha muonekano mzuri wako kwa afisa uajiri. Utakaposhindwa kutulia na ukaanza kujibu kwa kejeli, basi kuna nafasi kubwa kuwa utaikosa kazi.Kumbuka makampunimengi yanashirikiana, hivyo afisa ajira wako anaweza kua na mahusiano na makampuni mengine ya kuajiri. Pia inawezekana kua usaili huo mgumu ni moja ya njia zinazotumiwa na kampuni kuchuja maombi ya kazi. Hii hasa inaweza kuwa kweli kama kampuni hiyo inataka mtu mwenye sifa za kutoa huduma kwa wateja. Mara nyingi kwenye soko “maigizo” haya hutokea kama njia ya kuchuja maombi bila wewe kujua, hivyo kuwa makini.

 

Kuwa Mtulivu

Kubaki mtulivu wakati wa mahojiano yaweza kuonekana kama jambo la kawaida, lakini ni jambo gumu. Afisa uajiri mkali anapo kuhoji, ni ngumu kuendelea kuwa makini. Jitahidi utulie na uonyeshe uwezo wako wa kutatua matatizo ili ufaulu usaili huo. Ukiwa umetulia, onyesha ujasiri wako kwa kujielezea vizuri. Hii inaweza kusaidia hata kupunguza ukali wa mahojiano na kukuwezesha kuyamaliza kwa urahisi.

Eleza Panapokuwa na Tatizo

Mtazamo wako kuhusu kazi au majibu yako yanaweza yakawa yamemchanganya afisa uajiri. Kama ni hivyo, basi usiogope. Badala yake, jielezee tena kutumia kauli zinazo eleweka. Kauli kama,`’Naomba nikufafanulie hili kiundani?” zianweza kukuokoa kwenye mahojiano. Zitasaidiakuondoa mashaka kwa afisa uajiri ili muweze kuendelea na mahojiano. Wakati mwingine kosa linaweza lisiwe la kwako. Kama ni hivyo basi mwambie afisa uajiri na muombe akuhoji kwa heshima.


Elewa Pale Unaposhindwa

Baadhi ya mahojiano ya kazi yanakuwa ni mabovu kiasi kwamba ni ngumu hata kuyamaliza. Unapoona yamezidi ubovu yakatize, kubali kushindwa. Pale unapoona mahojiano ya kazi yanakosa heshima au yanakudhalilisha ni bora kuyaacha. Muda wako na heshima yako vina thamani kubwa. Usikubali vitumike kiholela. Pia unaweza kuwasiliana na kampuni anayotokea afisa uajiri na kutoa maoni yako.

Ni rahisi kusingizia mahojiano ya kazi mabovu kuwa ndio chanzo cha kukosa kazi, lakini wewe pia una nafasi ya kuchangia vizuri kwenye mahojiano hayo. Tabia nzuri wakati wa mahojiano, uwezo wa kuwa mtulivu na uwezo wa kujibu maswali kwa ufasaha vitakusaidia kufaulu kwenye mahojiano yoyote yale ya kazi.