Friday, January 19, 2018

Kesi ya mhasibu wa Takukuru yaahirishwa>

Watuhumiwa wa kesi ya Utakatishaji wa fedha

Watuhumiwa wa kesi ya Utakatishaji wa fedha wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, Dar es Salaam jana wakisubiri kusomewa mashitka yao. Kutoka kushoto ni aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Godfrey Gugai, Yasini Katera, Leonard Aloys na George Makaranga. Picha na Ericky Boniphace 

Kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizoendana na kipato inayomkabili mhasibu mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai na wenzake watatu imeahirishwa baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa jalada la kesi hiyo limepelekwa Takukuru kwa upelelezi. Mbali na Gugai, washtakiwa wengine ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera wote wanakabiliwa na mashtaka 43 yakiwamo 20 ya utakatishaji fedha haramu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wakili wa Serikali, Simon Wankyo alieleza hayo jana mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba. Kesi hiyo iliahirisha hadi Januari 31. (Hadija Jumanne)

-->