Mizani 600 ya pamba yakaguliwa Shinyang

Muktasari:

  • Sambamba na ukaguzi huo unaokusudia kuondoa dhulma waliyokuwa wanafanyiwa wakulima, wakala huo unawajengea uwe,zo wananchi kuitambua mizani inayofaa kwa biashara.

 Katika maandalizi ya msimu ujao wa mavuno ya pamba, Wakala wa Vipimo (WMA) mkoani Shinyanga imeshakagua mizani 600 kati ya 2,000 ilizopanga kuzifikia mwaka huu.

Sambamba na ukaguzi huo unaokusudia kuondoa dhulma waliyokuwa wanafanyiwa wakulima, wakala huo unawajengea uwezo wananchi kuitambua mizani inayofaa kwa biashara.

Meneja wa WMA mkoani hapa, Eliasi Nyanda alisema kwamba wanafanya hivyo ili kuongeza tija kwa mkulima. “Mizani zote zilizokaguliwa zina stika ili iwe rahisi kwa wakulima kuzitambua na kuruhusiwa kutumika kwa biashara kwa mwaka husika,” alisema.

Licha ya Shinyanga, Nyanda alisema elimu hiyo pia inatolewa kwa wakulima wa mikoa yote inayolima pamba ikiwamo Mwanza, Geita, Mara, Kagera, Simiyu na Tabora.

Mkulima wa pamba wilayani Kahama, Ndulu Shitinde alisema wizi wanaofanyiwa na wanunuzi wa pamba hivi sasa utakwisha.

“Hii ni elimu ya kufutwa wezi,” alisema.