Serikali yapiga marufuku kahawa kukusanywa kiholela

Muktasari:

  • Amesema vyama vya ushirikia ndivyo vinavyoaminiwa zaidi na ndivyo vilivyopewa jukunu la kupeleka katika masoko.

 Serikali imetangaza kuwa kuanzia sasa ni marufuku kahawa kukusanywa na watu wengine zaidi ya vyama vya ushirika.

Waziri wa Kilimo Dk Charles Tzeba ametoa kauli hiyo leo, Machi 23 wakati akifungua mkutano wa tisa wa wadau wa kahawa unaofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.

Dk Tzeba amesema lengo ni kudhibiti madeni wanayoingiziwa wakulima pamoja na 'kangomba' akisisitiza kuwa Serikali inaamini ushirika kuwa ndiyo mkombozi wa wakukima.

Amesema vyama vya ushirikia ndivyo vinavyoaminiwa zaidi na kuwa vyama ndivyo vilivyopewa jukunu la kupeleka katika masoko.

"Nasikia kuna minong'ono huko kuhusu kuwepo watu wanaojipitisha kwamba watawasaidia, hilo halipo bali Serikali imekubali kufufua ushirika kuanzia ngazi ya kijiji ili kumsaidia mkulima, " Amesema Tzeba

Katika hatua nyingine Tzeba ameionya moja ya kampuni mkoani Kilimanjaro ambayo imeanza kusambaza fedha kwa wakulima kwa ajili ya msimu akisisitiza kuwa ikithibitika lazima ataifutia leseni kampuni hiyo.