Wakulima wa mihogo waomba kutafutiwa soko

Muktasari:

  • Walisema hayo walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe katika mashamba yao yaliyopo Kata ya Kwamsisi kwa lengo la kusikiliza changamoto wanazokutana nazo.

        Handeni. Wakulima wa Muhogo wilayani hapa Mkoa wa Tanga, wameiomba Serikali kuwakopesha matrekta na kuwatafutia soko la uhakika baada ya kupata mavuno mazuri katika msimu wa kilimo uliopita.

Walisema hayo walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe katika mashamba yao yaliyopo Kata ya Kwamsisi kwa lengo la kusikiliza changamoto wanazokutana nazo.

Mkulima Bakari Sekilindi alisema mwamko ni mzuri kwa kuwa wakulima wengi ila Serikali iwatafutia soko la uhakika.

Mkuu wa wilaya hiyo, alisema utaratibu wa kuwaisidia wakulima hao umeanza kwa kuwatafutia mbegu bora ikiwamo kupewa elimu ya kilimo cha kisasa.

(Rajabu Athumani)