Waongoza utalii waanza kuhakikiwa

Muktasari:

Uhakiki huo, unafanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla ambaye alisema ili kuboresha utendaji kazi na usalama wa watalii, wote wanaotoa huduma za utalii watasajiliwa.

Arusha. Wizara ya Maliasili na Utalii, imeanza uhakiki wa sifa za waongoza watalii ili kuwezesha kuanza mfumo mpya wa kuwatambua na kuwasajili.

Uhakiki huo, unafanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla ambaye alisema ili kuboresha utendaji kazi na usalama wa watalii, wote wanaotoa huduma za utalii watasajiliwa.

Akizungumza na Mwananchi jana Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii (TTGA), Khalifa Msangi alisema kutokana na maagizo ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wameanza kukusanya sifa za waongoza watalii wote na kutuma wizarani.