Wateja Airtel Money kugawana shilingi bilioni mbili

Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu mgao wa gawio la faida ya shilingi bilioni 2 kwa wateja na watumiaji wa huduma ya Airtel Money. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Isack Nchunda.

Muktasari:

Fedha hizo ni sehemu ya faida ambayo kampuni hiyo ya simu imeipata kupitia huduma za airtel money

 

Dar es Salaam. Wateja wa airtel money nchi nzima wamepatiwa tabasamu kipindi hiki kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka baada ya kampuni ya airtel Tanzania kitangaza kuwa imetenga Sh2 bilioni kwa ajili yao.

Fedha hizo ni gawio ambalo kampuni hiyo ina utaratibu wa kulitoa kwa wateja wake kupitia sehemu ya faifa inayopata kupitia huduma za airtel money.

Taarifa ilitolewa leo Novemba 21 na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso imethibitisha kuwa gawio la faida kutokana na huduma ya Airtel Money hutolewa katika kila robo ya mwaka.

Gawio la kwanza lilianza kutolewa Mwaka 2015 na hadi kufikia leo hii jumla ya Sh11.8 bilioni zimeshagawiwa kwa wateja wa Airtel Money.

“Kila mteja wa Airtel Money hupata sehemu ya gawio hilo kulingana na salio linalosalia  katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku,” amesema Colaso na kubainisha kuwa gawio hilo linalotokana na faida iliyopatiikana kuanzia mwezi Juni hadi Septemba 2017.

“Tunajisikia furaha sana kugawa gawio hili ambapo kila mteja wa Airtel Money tapata na kisha mteja mweyewe ataamua kuitumia pesa yake atakavyo iwe kununua bando, muda wa maongezi, kulipia LUKU au kufanya malipo ya bili za huduma mbalimbali,” ilieleza taarifa hiyo.