Fid Q, Nature, Tip Top kula sikukuu Moro

Fid Q

Muktasari:

“Matamasha haya yatafanyika kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania, wateja wetu na Watanzania kwa jumla watapata burudani na elimu juu ya huduma zetu,” anasema Mmbando.

Dar. Wasanii wa wamuziki wa kizazi kipya, Fid Q, Juma Nature, Ney wa Mitego na kundi zima la Tip Top Connection ni miongoni mwa wasanii watakaopamba tamasha la Airtel maarufu kama Airtel Yatosha litakalofanyika kwa nyakati tofauti mikoa yote ya Tanzania.

Tamasha la kwanza litafanyika Jumapili na Jumatatu mjini Morogoro lengo likiwa kutoa burudani na kuielimisha jamii kupitia wasanii.

Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando anasema wameamua kutoa burudani wakati huu wa msimu wa sikuuu ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma yao mpya Airtel yatosha kwa Watanzania.

“Matamasha haya yatafanyika kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania, wateja wetu na Watanzania kwa jumla watapata burudani na elimu juu ya huduma zetu,” anasema Mmbando.

Kwa mujibu wa Mmbando tamasha la Airtel atosha litaanza kwenye viwanja vya sabasaba mjini Morogoro ambapo burudani itaanza kutolewa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 12 jioni na hakutakuwa na kiingilio.

Naye kiongozi wa Tip Top connection, Madee  anasema “Kama kawaida tumejipanga kuwapa wateja wa Airtel na Watanzania burudani ya Ukweli katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, tunaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika matamasha haya ya Airtel Yatosha. Airtel hivi karibuni imezindua huduma ya Airtel Yatosha inayomwezesha  mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu.