Muktasari:
Daddy Yankee anaungana na Jennifer Lopez ambaye naye majuzi alitangaza kuchangia dola za Marekani 1 milioni.
Baada ya kimbunga Maria kukipigi kisiwa cha Puerto Rico, mastaa mbalimbali wamejitokeza kuchangia na jana mwanamuziki Daddy Yankee ametangaza kuwa atatoa kiasi cha dola za Marekani 1 milioni kwa aajili ya kuchangia shughuli za uokoaji.
Daddy Yankee anaungana na Jennifer Lopez ambaye naye majuzi alitangaza kuchangia dola za Marekani 1 milioni ambazo ni wastani wa Sh2.4 bilioni.
Mbali na kiasi hicho Daddy Yankee ameahidi kutoa dola laki moja kwaajili ya Shirika la Red Cross ambalo linafanya kazi ya uokoaji.
Pi a amewaomba mashabiki kuendelea kutoa michango kwa kuwa wakazi wengi hawana huduma muhimu kutokana na miundo mbinu kuharibiwa vibaya.