Samsung Gear 360 inapiga Selfie mbele na nyuma

kamera aina ya Samsung gear 360

Muktasari:

Samsung   gear 360 inakupigia picha kwa mbele na nyuma. Kama upo ufukweni itapiga mawimbi yanayoonekana nyuma yako na mnazi ulipo mita chache kutoka yanapoishia maji.

Labda upo mapumzikoni na ungetamani kupata picha nzuri zitakazoipamba akaunti ya Instagram. Kama hilo ndilo hitaji lako basi kamera hii ndogo aina ya Samsung Gear 360 ndio jibu sahihi.

Simu yako inaweza kupiga picha lakini itabidi ugeuke mara mbili mbili kupata mwonekano wa mbele na nyuma.

Samsung   gear 360 inakupigia picha kwa mbele na nyuma. Kama upo ufukweni itapiga mawimbi yanayoonekana nyuma yako na mnazi ulipo mita chache kutoka yanapoishia maji.

Mtindo wa kupiga picha nyingi na kuzituma kwa pamoja unachukua chati na kwa kuwa kamera hii unaweza kuiunganisha kwenye simu yako unaweza kuzituma picha moja kwa moja na zote zikaonekana kwa wakati mmoja.

Kamera hiyo inayouzwa kuanzia dola 295 ambazo ni wastani wa Sh500,000 ni ndogo na inabebeka kwa urahisi ukilinganisha na kamera nyingine.